Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu The Zanzibar Revolution and Its Aftermath, Anthony Clayton, “tarehe 2 Januari [1964] mivutano ndani ya A.S.P. ilikamilika pale walipojiuzulu Othman Sharif, Hasnu Makame, Idris Wakyl na Saleh Saadalla.”32 Bwana George Mooring, katika barua yake ya tarehe 29 Agosti, 1963, kwa W. B. L. Monson wa Ofisi ya Makoloni, London, ameandika kuwa:
Imeripotiwa kuwa Moshe Feinsilber, Yahudi mwenye kuendesha biashara ya samaki hapa [Zanzibar], amejishughulisha na siasa kwa kuiunga mkono A.S.P. na yumo kujaribu kuwavutia viongozi wakubwa wa chama waachane na Abeid Karume na waungane na Othman Shariff katika jitihada zake za kuungana na Z.P.P.P. Ijapokuwa kikawaida maoni yake huwa yana uzito ndani ya chama, yeye [Finsilber] pia ameshindwa kukipeleka chama kwa Othman Shariff. Wakati huu viongozi wa A.S.P. wamekuwa wakitembelea Dar es Salaam mara kwa mara kwa kupata ushauri, ambapo imeripotiwa kuwa washauri wao wakubwa ni Kawawa na Kambona. Inasemekana kuwa Watanganyika wameshinikiza kuwa endapo Z.P.P.P.