Wanajua Maisha Ni Burudani, Hawachukulii Kila Kitu Siriasi
Kwao ni kama walikutana jana, hata kama washazeeka kwenye ndoa, bado wanataniana, bado wanatoka pamoja, wanacheza pamoja na kufanya mambo yote ambayo huko awali walikuwa wakiyafanya. Hawasingizii majukumu na kukasirika kasirika, wanaamua kuwa na furaha kila wakati, huchukulia changamoto kama shemu ya maisha.