Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hawakosoani Wanarekebishana

Wanajua namna ya kuongea, mwenza akikosea badala ya kumkosoa kwa dharau huzungumza na kueleweshana. Wanajua kuwa mtu huelewa zaidi pale unapoonge anaye taratibu, hawajifanyi kama wanajua kila kitu na kila wakati wapo tayari kujifunza. Hakuna maneno ya ukali wala kisirani, ukosoaji huwa ni wa kurekebisha na kufundishana
 
Wanaongea Kuhusu Pesa

Wanajua kua matatizo mengi ya ndoa husababishwa na pesa, hivyo huweka mipango mizuri kuhusu matumizi ya pesa zao. Ni wawazi katika vipato vyao na wanapanga namna ya kutumia pamoja. Hakuna mwenye nguvu zaidi katika kupanga matumizi ya vipato vyao hata kama havilingani au mmoja hachangii kipato kabisa.
 
Hawawazii Mabaya Wenza Wao

Watu wenye furaha ni wale ambao huwaza mazuri kwa wenza wao, hawana mawazo hasi kuhusu wenza wao. Kwa mfano mwenza wao anapochelewa kurudi huwaza labda kazi zimemzidi au kuna kitu cha maana anakifanya kuliko kuanza kuwaza labda anachepuka. Kumuwazia mabaya mwenza wako hata kama hajalifanya utaumia kama vile amefanya na itaondoa amani ndani ya nyumba.
 
Wanawasiliana

Wanajua wenza wao si malaika kwamba watajua wanachowaza, mmoja akitaka kitu kwa mwenza wake hasubiri mwenzake kubuni au kufikiria sana, humuambia na kama hakiwezekani basi anaridhika. Mwenza wako si mnajimu kwamba kila wakati atajua unawaza nini au unataka nini, muambie unachohitaji ili akufurahishe.
 
Hawajipangii Majukumu ya Kudumu


Kwenye ndoa kila kitu nikusaidiana, kwamba watu wenye furaha hawapangiana kazi kama ofisini kwamba mke ni lazima apike, afue au afanye usafi. Mume nilazima kutoa hela ya chakula, ada na vitu vingine. Wao hufanya chochote, mke anaweza lipa ada akanunua chakula bila kinyongo, mume akaamua kupika au kuosha vyombo. Kwakifupi hufanya mambo kama wenza na si kwa kutegeana eti kusema hii ni kazi ya flani?
 
Wanasaidiana; Yaani badala ya kulaumu tu na kulalamikia kuwa mbona wewe hujafanya hiki na yule hajafanya kile wao husaidiana katika majukumu. Mmoja akiona kitu hakiko sawa, akiona mwenzake hajamaliza au hayuko vizuri kufanya kitu flani basi hukifanya bila kinyongo kwa furaha ya kumsaidia mwenza.
 
Wanashukuru

Kila mmoja anatambua majukumu ya mwenzake na namna anavyojitahidi kumfurahisha mwanzake. Wanashukuru kwa kila kitu, hawashukuru tu kwa maneno bali pia kwa vitendo na kutoa tabasamu, hata kama ni kwa kitu kidogo tu ambacho mmoja wao atamfanyia mwingine lakini watashukuru pamoja.
 
Wanafanya Mambo Mengi Kwa Pamoja

Wanajua kuwa ndoa ni pamoja na kushirikiana kufanya mambo pamoja. Si katika majukumu ya kifamilia tu bali hata katika mambo mengine kama michezo na burudani. Hutembea pamoja, kufanya mazoezi pamoja, kula pamoja, kuangalia mpira pamoja na kufanya angalau kitu kimoja kwa pamoja kamka wanandoa.
 
Wanaungana Mkono

Iwe ni katika kazi au hobi, watu wenye furaha huungana mkono hata kama hawafurahii kile ambacho wenza wao wanakifanya lakini kwakuwa wanajua kuwa kinawapa furaha basi huungana mkono. Mwanamke ambaye hapendi mpira atamsindikiza mumewe uwanjani kama ambavyo mwanaume ambaye hata hajui urembo ni nini atampeleka mkewe kwenye mashindano ya urembo.
 
Wanasameheana Na Kusahau

Hawakumbushani mambo yaliyopita, wakishasamehe basi husahau na hata mmoja wao akirudia kosa lile lile basi hawatasema hii ndiyo tabia yako bali watarekebishana na kusonga mbele. Hawaweki kumbukumbu ya makosa ya wenza wao na hawana vinyongo, hutoa madukuduku yao kwa kuongea na si kwa kulalamika pembeni na wakishaonge abasi husahau.
 
Kila mmoja anatambua udhaifu wa mwenzake

Kila mmoja anamjua mwenzake vizuri anatambua udhaifu wake na amekubaliana nao, kuishi nao na pia kumsaidia mwenza wake kutokana na udhaifu huo. Hamsengenyi wala kumnyanyapaa mwenzake kutokana na ushaifu huo. Atamsaidia mwenza wake kuficha ushaifu huo na kuonyesha mbele za watu kuwa mwenza wake ni mkamilifu.
 
Wanasali Pamoja

Labda hii ilipaswa kuwa ndiyo sifa ya kwanza lakini nimeiweka mwisho ili kuonyesha kuwa yote hayo hayawezi kuwezekana bila Mungu. Watu wenye furaha wanamjua Mungu na mioyo yao inaamani kwanni wanajua kua kuna nguvu ya ziada ambayo inawalinda.
 
Interesting facts:

The coca-cola name in China was first read as "Ke-Kou-Ke-La",
meaning "Bite the wax tadpole" or "female horse stuffed with wax", depending on the dialect.
Coke then researched 40,000 characters to find a phonetic equivalent "Ko-Kou-Ko-le",
transilating into "happiness in the mouth."
 
Back
Top Bottom