Pia, tukiwaangalia tunadhani wana furaha ndani yao lakini nimepata bahati ya kuzungumza na wengi wa aina hii na kugundua kuwa hawakuwa na furaha ya maisha yao kama wengine walivyofikiri
kwa mfano; hali mbaya ya mahusiano baina yako na umpendae, matatizo ya tabia za watoto wako, matatizo ya kazini kwako, kushindwa kufikia malengo binafsi, historia yako binafsi, maumivu ya moyo, mambo ya ndugu na mengine mengi
Wengi tumejikuta katika matatizo sababu tu ya kuingilia mambo yasiyokuwa yetu, tunafanya hivyo sababu mara nyingine tunafikiri tunavyojua sisi ndio sawa, na mtazamo wetu ndio uko sahihi zaidi, na yeyote asiyeafikiana na mtazamo wetu anastahili kupingwa.
Matokeo yake wengine wanakosa usingizi, wanapata vidonda vya tumbo, wengine shinikizo la damu (BP) n.k. Chuki au maumivu haya ya moyo yalifanywa mara moja, lakini matokeo yake yanaeendelea kuharibu maisha na afya kwa muda mrefu kwa sababu tu ya wewe kuikumbuka chuki au uchungu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.