Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
Tunda hili la tende limesheheni utajiri wa kiafya ya binadam Baadh ya utajiri uliopo katika tende Wanga, Vitamin B1 B2 B3, Protini, nyuzi nyuzi (fibers), Magnesium, potassium na mafuta hizi ni baadh ya vilivyomo katika Tende
 
KWA WANAWAKE WAJAWAZITO.

Mwanamke mjamzito akila tende ni chakula kizuri sana kwake humfanya awe na afya nzuri yeye na mtoto alie tumboni
 
Mwanamama mjamzito anatakiwa kutumia tende kama chakula katika kipindi chote cha ujauzito au ikiwa bado wiki au mwezi kabla ya kujifungua hii humsaidia kwa kumrahisishia kuzaa kwa wepesi lakini pia wakati anapokuwa na uchungu humsaidia kupunguza makali ya uchungu wa uzazu Ulaji wa tende kwa mama mjamzito humsaidia pia katika kukuza kizazi na kutomfanya amwage dam nyingi wakati wa kujifungua na hata baada ya kujifungua anatakiwa aendelea kula kwasabab ya kumuondolea maumivu ya uzazi pamoja na kusafisha kizazi
 
MMENG'ENYO WA CHAKULA

Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.
 
UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha. Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
 
KUUPA NGUVU MWILI

Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima.
 
NZURI KWA AFYA YA UBONGO

Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke
 
NZURI KWA AFYA YA MOYO

Tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol). Hivyo ni nzuri kwa wenye shinikizo la damu (high / low blood pressure)
 
Back
Top Bottom