Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KUONGEZA DAMU MWILINI

Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka / kupungukiwa damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini.
 
DAWA YA UNENE

Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa.
 
KUFUNGUA CHOO

Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, kunywa juice ya tende na choo kitafunguka na kuwa laini. Pia kwa wenye matatizo ya kupata Choo chepesi mno (kuharisha) tatizo litakwisha
 
KUBORESHA NURU YA MACHO

Tende vile vile ina vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa kuimarisha nuru ya macho na kuondo tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
 
Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi na nyingine nyingi.
 
Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.


Katika hekima hii inatuonyesha katika maisha, unaweza ukamfanyia mtu kitu ambacho kitagusa maisha yake pasipo kujali kitu hicho ni kibaya au kizuri, lakini kumbukumbu inakuwa inabaki sana kwa yule aliyeguswa na alichofanyiwa.
 
Ndio maana unaweza ukamsaidia mtu usikumbuke, unaweza ukamfanyia mtu ubaya usikumbuke, lakini yule aliyefanyiwa ubaya huo anakuwa anakumbuka sana. Hapa ukumbuke tunaaswa kuwa makini yale yanayogusa maisha ya wengine.
 
Jiulize ni mara ngapi au kuna wakati uliwahi kumfanyia mtu kitu fulani ambacho kilimsaidia, utakuta muda unakuwa umepita na wakati huo umesahau, lakini unapokutana na mtu yule anakukumbusha na kukwambia unakumbuka ulinifanyia kitu hiki.
 
Mara nyingi wengi wetu hubaki tukishangaa kwa kukumbushwa kitu kile. Kwa hiyo unaona hata ubaya ukimfanyia mtu ni hivyo hivyo. Kwa wewe ukiyefanya ni rahisi kusahau lakini si kwa ,mtu aliyefanyiwa ubaya huo hata kidogo hawezi sahau.
 
Hapa ndipo unaweza ukapata picha kwa nini shoka halikumbuki mti liloukata na kwa nini mti uliokatwa hulikumbuka shoka. Unaona mti unakumbuka shoka kwa sababu shoka liligusa maisha ya mti huo kwa namna fulani.
 
Maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri.
Ni kawaida sana maneno mabaya kuweza kuenea kwa haraka kuliko maneno mazuri. Unaweza ukafanya mengi mazuri lakini ukikosea kidogo maneno hayo yatasambaa sana kuliko ambavyo hukutarajia iwe hivyo
 
Hapa kupitia hekima hii inatunaonyesha wazi kwamba maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri, hilo ni la ukweli na halina ubishi. Mwangwi wa kitu kibaya unasikika zaidi kuliko mwangwi wa kitu kizuri.
 
Angalia kipindi ambacho ulifanya ubaya, mwangwi wake ulisikika vipi na kipindi ambacho ulipofanya mazuri mwangwi wake ulisikikaje pia. Hapo utagundua kipindi ambacho ulifanya mabaya mwangwi wake ulionea sana.
 
Fanyia kazi hekima hizi naamini kwa sehemu zitakuwa zimekusaidia kutoka hatua moja na kulekea hatua nyingine ya maisha yako. Kila wakati hekima zinakupa busara, hekima zinakuza uelewa wako kwa namna fulani.
 
Safiiii sana hiyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…