Fernandez tayari amekwisha fanya mazungumzo na Manchester United na Real Madrid na hivi karibui ametoa kipengele cha eurp milioni 20 (£16.6m). (Express via Cesar Luis Merlo - in Spanish)
Aberdeen wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kumchukua mlinda lango wa klabu ya Ipswich Town mwenye umri wa miaka 31 kutoka Czech Vaclav Hladky, ambaye awali alicheza chini ya Dons boss Jim Goodwin katika St Mirren. (Record)
Arsenal na Newcastle kwa pamoja zinahusishwa na kiungo wa kati wa klabu ya Ufaransa ya Lyon -Lucas Paqueta, 24. Mchezaji huyo wa kimataifa wa The Brazil awali alihusishwa na taarifa za kuhamia Paris St-Germain na - gharama ya kumnunua ni pauni milioni 58. (Chronicle)
West Ham na Wolves zitatakiwa kulipa euro milioni 70 (£58.1m) ili kutimiza kigezo cha kipengele cha kumuachlia winga Lucas Ocampos, 27, huku klabu ya Uhispania ikiwa tayari kurefusha mkataba wake kwa mwaka mmoja na kuongeza gharama ya kipengele cha kumuachilia hadi euro milioni 90 (£74.7m). (Super Deporte)
Arsenal wanaandaa ofa ya euro milioni 20 (£16.6m) kwa ajili yaw inga Mturuki kutoka Galatasaray Kerem Aktürkoğlu mwenye umri wa miaka 23. (Star Gazetesi - in Turkish)
Brentford wanamatumaini mchezaji maarufu wa Denmark Christian Eriksen ataendelea kubaikia katika klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miezi sita, lakini wanakabiliwa na "ushindani mkali" katika kupata Saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miakaa 30 kutoka timu yake ya zamani ya Tottenham. (90Min)
Mholanzi huyo mwenyeumri wa miaka, 52, anatarajiwa kujiunga nao kwa mkataba wa miaka minne, lakini tangazo halitatolewa kabla Ajax kukabiliana na PSV Eindhoven katika mchezo wa fainali ya kombe la Uholanzi Jumapili. (Athletic - subscription required)
Manchester United pia wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa RB Leipzig na Ufaransa Christopher Nkunku, 24, ambaye amefunga magoli 17 na kusaidia kufungwa kwa magoli 12 katika mechi 29 za msimu huu za ligi ya Ujerumani Bundesliga . (Florian Plettenberg)
Manchester United na Tottenham kwa pamoja zina nia ya kusaini mkataba na mlinda lango wa West Brom na England mwenye umri wa miaka 29- Sam Johnstone msimu huu. (Sky Sports)
Liverpool wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 25 kwa ajili ya mlinzi Mbrazili kutoka klabu ya Torino- Gleison Bremer ambapo Januari tayari walikuwa wameelezea nia yao kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 25. (Tuttomercato - in Italian)
Napoli wameazimia kuendelea kumshikilia mfungaji wa mabao zaidi katika klabu hiyo Victor Osimhen msimu huu licha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kusakwa na klabu za Manchester United na Arsenal. (Teamtalk)
Aston Villa wameelezea nia yao katika kiungo wa kati -nyuma wa Ujerumani Matthias Ginter, ambaye mkataba wake katika Borussia Monchengladbach unamalizika mwishoni mwa msimu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.