Kijana wa Nairobi nchini Kenya, Alvin Linus Chivondo (22) amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuiba chakula na bidhaa nyingine Naivas Supermarket licha ya Kijana huyo kujitetea kwamba aliiba kutokana na hali ngumu ya maisha, njaa na pia alitaka chakula cha kwenda kulisha Familia yake. Alvin amehukumiwa kwa kuiba mchele kg 5, lita 5 za mafuta ya kula, sukari kilo 2 na bidhaa nyingine ambavyo vyote kwa ujumla vina thamani ya Ksh. 3,165 (Tsh. 63,977) Mahakama ya Sheria Milimani imesema Alvin alifanya kosa hilo April 10,2022 ambapo ili kukwepa kifungo ilimpa Alvin adhabu ya kulipa faini ya Ksh. 100,000 (Tsh. 2,021,394) ambayo hata hivyo alishindwa kuilipa na kupelekwa gerezani.