Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wawindaji wanne wametiwa nguvuni na mamlaka ya uhifadhi wa misitu Nchini India Maharashtra, kwa tuhumza za kumbaka kenge kwa zamu (gang-raping). Katika taarifa iliyotangazwa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa tukio hilo limebainika baada ya kufanya uchunguzi kwenye simu za wawindaji hao haramu (4), baada ya uchunguzi waliona Picha za Video wakifanya kitendo hicho ambacho kimepekea watu walio wengi kukumbwa na mshangao. Awali wawindaji hao walianza kutiliwa shaka na Mamlaka hiyo, ndipo wakaanza kufuatiliwa kupitia kamera maalum (cctv), zilizopo hifadhini humo. Inaelezwa kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika watu hao watachukuliwa hatua za kisheria, ambapo kifungo cha juu zaidi kwa kosa hilo ikitajwa huwa ni miaka 7 gerezani. Kenge aliebakwa kwa zamu ni aina ya kenge wakubwa wanaojulikana kama bengal monitor lizards, ambao ni moja ya viumbe vinavyolindwa sababu ya kuwa hatarini kutoweka katika uso wa dunia.
 
Amka mapema
Unapoamka mapema husaidia siku yako kwenda vizuri kwa kuwa utapata muda wa kutosha wa kupangilia mambo yako. Hivyo ni vyema ukalala mapema na kuamka mapema ili mwili wako uweze kupata mapumziko mazuri kwa ajili ya kazi za siku inayofuata.
 
Sala/ Maombi
Kusali ni muhimu kwako na wakati huo huo pia utakuwa ukiipatia akili yako hali ya ukimya. Unaposali kutokana na imani yako kwa kiasi kikubwa husaidia kufungua milango yako ya baraka katika shughuli zako za siku husika
 
Soma Kitabu

Licha ya kwamba si utamaduni wa wengi wetu wa kusoma hasa asubuhi, lakini ni wakati mzuri zaidi wa kuingiza mambo mazuri kichwani kabla ya kelele za dunia hazijaanza. Hakikisha vitabu unavyosoma ni vile vyenye kukupatia maarifa.
 
Andaa ratiba ya siku yako
Epuka kuanza siku yako bila ratiba kwani ni sawa na kuanza safari ya kuelekea usikokujua. Orodhesha mambo utakayofanya katika siku hiyo.
 
Chukua dakika tano tu kujiuliza maswali yafuatayo kisha ujijibu kwa haraka:

(1) Ukipata million 200 saizi utafanyia nini?

(2) Je, kama ukiwa umepokea hiyo million 200 alafu baada ya miezi 5 ukafilisika Mali zote itakuwaje?

(3) Ni nini unauhakika utabaki nacho hata ukifilisika?

Baada ya zoezi hilo naenda kukueleza kitu kuhusu pesa ambacho kitakufanya ujijue wewe ni Masikini au Tajiri kulingana na aina ya majibu yako;
 
MONEY IS AN IDEA:

Hakuna hela bila wazo, hela inafuata mfereji uitwao IDEA. Wazo la mtu mmoja linaweza kunufaisha watu wengi wakapata pesa. Fikiri, njia yoyote au kazi yoyote unayoifanya je kusudi lake nini? Kusudi hilo utagundua ndilo lilipelekea ubunifu(idea) wa kazi hiyo. Mfano: alie buni kuweka hela bank alianza na idea lakini idea hii imepelekea watu kuajiriwa kama wafanya kazi aidha uhasibu au hata mlinzi wa bank lakini yote ilianza kwa wazo la mmoja au wachache.
 
MONEY HAS A PLAN:

Hii ndio naiita "mchezo wa pesa/The money game". Kuna jamaa alishawahi fikia hatua ya kusema hela ni roho (money is a spirit) kutokana na mchezo huu, kila masikini hulalamika na kusema wakipata pesa haikai! Hii ni sababu pesa inamipango yake pia (money has its plan) ambao ni "To come and Go/kuja na kuondoka". Pesa haina na haitakuja kuwa na tabia ya kusimama, siku zote hutembea. Tofauti ya masikini na tajiri ni; masikini hujaribu kuweka hela ili iwe nyingi wakati tajiri hutengeneza njia itayo muwezesha kuizungusha hela ili izidi kuongezeka.
 
SAVERS ARE LOOSERS:

Huu msemo nimeutoa kwa moja ya mentors wangu ukimaanisha wanaohifadhi pesa siku zote huzipoteza. Kama nilivyo kwisha sema, pesa ina asili ya kuzunguka hivyo huwezi ihifadhi bank bila kuitengenezea mzunguko kwanza, ni lazima utaitumia na mwishowe kuipoteza.
 
ALWAYS PLAN FIRST:

Siku zote kuwa na mipango kabla ya kuwa na hela. Usisubiri upate pesa ndio uanze kupanga. Ndio swali lile la kwanza kabisa, tajiri ukimpa million 200 anajua ataizungusha vipi tayari. Lakini masikini ukimpa hela hiyo atapata kichaa kwani akiri yake haijazoeshwa kuwa na mipango hata ya pesa ambayo bado hana.
 
Zifuatazo ni faida au taswira chanya za kukosea;

KAMA HUKOSEI BASI UNAKOSEA: Inaweza kuwa ngumu kuelewa, ili ujue unachokifanya kinafanyika kiusahihi basi hunabudi kukabiliana na makosa. Mtoto anaejifunza kutembea huanguka Mara kadhaa na kuanguka kwake kutokana na makosa huwa mwalimu wake. Nasema hivi kwasababu huwezi jua jambo lolote na kulifanya kwa ubora bila kukosea.
 
Back
Top Bottom