Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usikebehi taasisi za kijamii.

Hata kama hukubaliani na mtu au watu, usiwakebehi, kuwadharau au kuwakosoa kwa namna ya kudhalilisha. Hii inakwenda kuanzia kwenye taasisi mbalimbali kama za kidini na hata kwa watu binafsi.
 
Jichukulie kama mtu ambaye una jukumu la kumsaidia.

Tunapopewa kazi ya kuwasaidia wengine, tunafanya kazi nzuri sana, lakini kwetu sisi wenyewe hatufanyi kazi nzuri. Jichukulie wewe kama mtu uliyepewa jukumu la kumsaidia kisha msaidie hasa.
 
Waombe watu wakusaidie kitu kidogo ili nao wakuombe uwasaidie kitu.

Maisha ni mahusiano, kadiri mahusiano yako na wengine yanavyouwa bora, ndivyo maisha yako yanavyokuwa bora. Na mahusiano yanaimarishwa kwa namna watu mnashirikiana na kusaidiana, waombe watu wakusaidie kitu, ili nao wawe tayari kukuomba uwasaidie kitu.
 
Usijaribu kumwokoa mtu ambaye hataki kuokolewa, na kuwa makini unapomwokoa mtu ambaye anataka kuokolewa.

Kuna sababu kwa nini mtu ameingia kwenye matatizo ambayo unamwona anapitia. Ukikazana kumwokoa mtu ambaye yupo kwenye matatizo, bila ya kujua sababu iliyomwingiza kwenye matatizo hayo, unajiingiza mwenyewe kwenye matatizo.
 
Hakuna kitu kilichofanywa vizuri ambacho hakina maana.

Kitu chochote ambacho kimefanywa vizuri, hata kama ni kidogo kiasi gani, kina maana kubwa sana. Fanya kila kitu vizuri, hata kama ni kidogo.
 
Iweke nyumba yako vizuri kabla hujakosoa dunia.

Kukosoa ni rahisi, lakini kuchukua hatua ni kugumu. Tunaishi kwenye dunia ambayo kila mtu anaweza kukosoa wengine, lakini yeye mwenyewe maisha yake yanamshinda. Nyoosha kwanza maisha yako kabla hujajipa jukumu la kuinyoosha dunia.
 
Vaa kama mtu unayetaka kuwa.

Ukishajua unataka kuwa nani, angalia jinsi watu hao wanavaa kisha vaa hivyo pia. Hata kama hujafikia ngazi hiyo, wewe vaa kama watu hao, na hilo litawafanya watu wakuchukulie kama mmoja wao na kukusogeza karibu na mafanikio yako.
 
Usiepuke kitu cha kutisha kinachokuzuia na usifanye mambo hatari yasiyo na umuhimu.

Kitu chochote kinachosimama kwenye njia yako ya mafanikio, na kukuzuia wewe kufika kule unakotaka kufika, unapaswa kukiondoa. Lakini pia kuwa makini usijiingize kwenye mambo hatari, ambayo hayana maana kwako
 
Usiwaruhusu watoto wako wafanye kitu kitakachokufanya uwachukie.

Kama una watoto, basi jua una jukumu la kuwalea vizuri kwenye msingi wa maadili, na hilo litahuisha kuwaadhibu pale wanapokosea
 
Usimgeuze mke wako kuwa kijakazi wako.

Watu wengi huishia kuwafanya wake zao kama wasaidizi wao wa kazi za nyumbani, hilo linapelekea mahusiano hayo kuwa na changamoto kubwa. Mke wako anapaswa kupata nafasi yake sahihi ya mke, ambayo ni mshauri na mshirika kwa kila unachofanya.
 
Usifiche vitu ambavyo havihitajiki kwenye ukungu.

Kuna vitu ambavyo vinatokea kwenye maisha yako, ambavyo huvitaki, lakini badala ya kuvikabili, unavificha kwenye ukungu, na kujifanya kama havijatokea. Kadiri unavyoficha vitu hivyo vinakuwa na baadaye vinaleta madhara makubwa. Kama kitu kisicho sahihi kimetokea, kinapaswa kusahihishwa na siyo kufichwa.
 
Usiwasumbue watoto wanapofanya vitu vinavyoweza kuonekana ni hatari.

Kama jamii tunawalinda sana watoto na kuwaondolea kila aina ya hatari, lakini hilo haliwasaidii katika kuwa watu bora. Watoto wanahitaji kujiweka kwenye mazingira ambayo ni hatari kwa kiasi, ili wanapokosea wajifunze kwa maumivu watakayopata.
 
Usikubali anayekuonea aendelee na uonevu wake.

Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu kuchukulia ni kitu cha kawaida, simamia utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi.
 
Andika barua kwa serikali kama unaona kitu ambacho kinapaswa kurekebishwa, na pendekeza suluhisho.

Hii ni bora kuliko kukaa na kulalamika kuhusu serikali inafanya au haijafanya nini. Andika barua kueleza kile ambacho siyo sahihi na pendekeza suluhisho, na hata kama barua yako haitafanyiwa kazi, basi mawazo yako ya kuisaidia serikali yatasikika na wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…