Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
Yafuatayo ni mambo 40 muhimu kuzingatia kwenye maisha

Sema ukweli.

Nafikiri hili halina haja ya maelezo marefu, sema ukweli mara zote, usidanganye hata kama ni kitu kidogo kiasi gani, sema kweli na kweli itakuweka huru. Ukweli ni rahisi kukumbuka na ukweli utakuweka sehemu salama mara zote.
 
Usifanye kitu unachokichukia.

Fanya unachopenda, penda unachofanya, huu ndiyo msingi wa maisha bora na ya mafanikio. Kama kuna kitu hutaki au hupendi kufanya usifanye, muda wako ni mchache na wa thamani, usiupoteze kwa yasiyo muhimu
 
Fanya kile ambacho ni muhimu kwako, na siyo ambacho ni rahisi.

Kila mtu anataka kukata kona, kila mtu anatafuta njia ya mkato ya mafanikio, kila mtu anatafuta njia ya kupata fedha bila ya kufanya kazi. Usiwe katika watu hawa, fanya kile ambacho ni muhimu kwako, na siyo kutafuta kilicho rahisi. Kwa sababu mwisho wa siku maisha siyo fedha tu, unaweza kuzipata na bado ukaona maisha hayafai.
 
Chukulia kwamba mtu unayemsikiliza kuna kitu anachojua ambacho wewe hujui.

Ukweli ni kwamba kila mtu kuna kitu anajua ambacho wewe hujui, hivyo unapofanya mazungumzo na yeyote, sikiliza kwa makini sana. Mtu yeyote atakuambia chochote unachotaka kujua, kama utasikiliza kwa makini.
 
Weka juhudi kuimarisha mahaba kwenye mahusiano yako.

Mahusiano ni kazi na kila kazi inahitaji juhudi. Kuweza kuwa na mahusiano bora na mwezi wako, unahitaji kuweka juhudi katika kujenga mahusiano hayo.
 
Fanya angalau kitu kimoja kuwa bora kila mahali unapoenda.

Usiende sehemu yoyote halafu ukaondoka hujabadili kitu chochote kikawa bora, itakuwa haina maana yoyote ya wewe kuwepo eneo hilo. Angalia kipi unaweza kuboresha zaidi popote ulipo, kisha boresha.
 
Tengeneza taswira ya unataka kuwa nani, kisha weka juhudi kufikia taswira hiyo.

Watu wengi hawajui nini wanataka kwenye maisha yao hivyo wanajiendea tu. Usiwe wewe, jua unataka kuwa nani, unataka kufikia wapi, kisha kila siku weka juhudi kufika pale unapotaka kufika.
 
Usijiruhusu kuwa na kiburi au hasira.

Hizi ni hisia mbili ambazo zitakuharibia sifa yako, kuvuruga mahusiano yako na wengine na kukuingiza kwenye matatizo makubwa, usikubali hisia hizo zikutawale.
 
Jaribu kufanya chumba kimoja kwenye nyuma yako kuwa kizuri iwezekanavyo.

Kwenye nyumba unayoishi, kazana kufanya chumba kimoja kuwa kizuri sana kiasi kwamba kila wakati utapenda kuwa kwenye chumba hicho, kisha kifanye kuwa eneo lako la kupumzika au kutafakari maisha yako
 
Jilinganishe na ulivyokuwa jana, na siyo kujilinganisha na wengine walivyo leo.

Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha yako, ni kujilinganisha na mtu mwingine yeyote, awe yupo juu yako, chini yako au sawa na wewe. Mtu pekee wa kujilinganisha naye ni wewe mwenyewe, kama leo umefanya kwa ubora kuliko jana unapiga hatua, kama umefanya kama jana unarudi nyuma, kama umefanya chini ya ulivyofanya jana hujui unachofanya.
 
Weka juhudi kubwa uwezavyo kwenye angalau eneo moja kisha angalia nini kitatokea.

Kwenye maisha yako, chagua eneo moja ambalo utaweka juhudi kubwa sana, utakwenda hatua ya ziada, utafanya kila kinachopaswa kufanyika, kisha angalia matokeo utakayopata, yatakuwa matokeo bora, makubwa na ambayo yatakupa hamasa ya kuendelea na juhudi zaidi kwenye maeneo mengine ya maisha yako.
 
Kama kumbukumbu za nyuma zinakufanya ulie, ziandike kwenye karatasi kwa umakini na ukamilifu.

Kumbukumbu tunazobeba, zinaweza kuwa mzigo mzito kwetu na unaoturudisha nyuma, tunahitaji kuutua. Kitendo cha kuandika kitu, unakuwa umekitua kutoka kwenye akili yako na kinaacha kuwa mzigo.
 
Imarisha muungano wako na watu.

Unahitaji kuwa na mtandao wa watu ambao wanaweza kukusaidia kwenye maeneo mbalimbali na wewe pia unaweza kuwasaidia. Imarisha muungano na mahusiano yako na wengine.
 
Back
Top Bottom