PSG itambakiza mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, kwa msimu mmoja zaidi lakini iko tayari kuruhusu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, leave. (Sky Sports News)
Juventus iko kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa Argentina Angel di Maria, 34 kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu baada ya kuamua kutoongeza mkataba wake. (Goal)
Stade Reims itamruhusu mshambuliaji mfaransa mwenye miaka 19 Hugo Ekitike kuondoka klabuni hapi kwa ada ya £30m msimu wa kiangazi na Newcastle wanatarajia kurejesha nia yao ya kumsajili baada ya kufanya mazungumzo na kinda huyo mwezi Januari. (Shields Gazette)
Ilkay Gundogan, 31, anasema angefurahi kumaliza soka lake Manchester City, lakini kiungo huyo wa Ujerumani angetamani kutimkia ligi ya Uturuki Turkish au MLS ya Marekani mkataba wake utakapomalizika mwaka 2023. (Sport 1, in German)
Neco Williams anasema hajua atacheza klabu gani msimu ujao. Mlinzi huyo wa kulia wa Wales mwenye miaka 21 kwa sasa anacheza kwa mkopo Fulham akitokea Liverpool. (Wales Online)
Chelsea huenda ikafufua tena mbio zake za kumnasa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, dirisha lijalo baada ya kuthibitishwa kuwa Antonio Rudiger ataondoka klabuni hapo. (Football London)
Kiungo wa kimataifa wa Brazil anayehusishwa na Newcastle Lucas Paqueta, 24, ameiambia klabu yake ya sasa ya Lyon kwamba atafanya uamuzi wa hatma yake mwishoni mwa msimu. (Evening Chronicle)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.