Real Madrid inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho kwa ajili ya mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, huku Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 29 akiwa tayari kuhamia Bernabeu kwa mkataba wenye mshahara wa angalau £200,000 kwa wiki. (Guardian)
Manchester City wanafikiria kumnasa kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23, ambaye amekuwa akisakwa kwa muda mrefu pia na mahasimu wao Manchester United na Chelsea. (Telegraph, subscription required)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 23, amekuwa akihusishwa nkutaka kuhamia Real Madrid katika majira ya kiangazi, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa hatatangaza rasmi kuhusu hatma yake mpaka baada ya mchezo wa mwisho wa klabu hiyo msimu huu dhidi ya Metz, Mei 21. (Marca)
Norwich City imeingia katika mbio za kumsaka kiungo muingereza wa Bristol City Alex Scott, huku Tottenham na Leeds tayari zinamfuatilia kinda hilo la miaka 18. (Football League World)
Barcelona wanaweza kukubali kumuachia Frenkie de Jong, 24, kuondoka kwa ada ya £58m, huku Manchester United ikionyesha nia ya kumtaka kiungo huyo wa Uholanzi. (El Chiringuito)
United inaweza kuwapa Barcelona mshambuliaji wake wa kimataifa wa England Marcus Rashford na mlinzi wa kushoto Mbrazil Alex Telles, 29 kubadilishana na De Jong. (Fichajes)
Meneja mpya wa Manchester United Erik ten Hag atafanya mkutano wa mtandao na mchezaji mmoja mmoja kutathmini nani atasalia au kuondoka kabla ya kushika mikoba mwezi Juni. (Mirror)
Mchezaji ambaye ni wazi anaondoka Old Trafford ni Paul Pogba, 29, na tayari kiungo huyo mfaransa ameshajiondoa kwenye kundi la WhatsApp la timu hiyo baada ya kupata ofa kutoka Real Madrid na PSG. (Mirror)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.