Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAFUA YA KIHISPANIA (mwaka 1918)

Mwishoni mwa Vita ya kwanza ya dunia ugonjwa huu uliibuka kisha ukasambaa kwa haraka duniani hasa katika kambi za jeshi za wakati huo
 
Haijathibitika kuwa ugonjwa ulitokea hispania lakini ulikuja kuisha mwaka 1919 mpaka muda huu dunia haijui ni kipi kilipelekea ugonjwa huu ukamalizika ghafla
 
ANTONINE (mwaka 165-180)
Inasemekana ugonjwa huu ulianzia huko nchini Mesopotamia katika mji wa Seleucia (Baghdad ya sasa) na ugonjwa huu ulisambazwa na wanajeshi ambao walikuwa wanatoka kwenye vita kurudi nchini kwao Roma

inasemekana ugonjwa huu uliua zaidi ya watu million 5
 
Zaidi ya watu elfu 2 kutoka Roma walifariki kila siku

Sababu ya ugonjwa huu kuitwa antonine ni kutoka kwa jina la mtawala wa Roma kwa wakati huo aliitwa Marcus Aurelius Antoninus naye alifariki kwa ugonjwa huo
 
MAFUA YA ASIA (mwaka 1957)
Ndani ya miezi 6 zaidi ya watu elfu 14 walifariki kwa mafua haya..inasemekana yalianzia Hong Kong kisha yakaenea China nzima kisha yakasambaa marekani na uingereza

katika awamu ya pili ya ugonjwa mwaka 1958 zaidi ya watu million 1 walifariki duniani kote
 
Back
Top Bottom