Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja na mambo mengine ni sehemu ya makaburi ya Giza yaliyokuwa mahali pa kuzika wafalme wa Misri na wakubwa wa milki yao kwa muda wa miaka 2500.
 
Ziko kando ya bonde la mto Nile, karibu na mji wa Giza takriban kilometa 15 kutoka Kairo, mji mkuu wa Misri.
 
AJABU LA 3: Hekalu ya Artemis mjini Efeso (Asia Ndogo)

Hekalu hilo lilihesabiwa kati ya maajabu saba za dunia.Lilijengwa mjini Efeso kwa muda wa miaka 120 kuanzia mwaka 560 KK.
 
Mfalme Kroisos wa Lidia ndiye aliyeanzisha ujenzi huu.Hekalu lilikuwa na urefu wa mita 115 na upana wa mita 55. Nguzo zake zilisimama mita 18.
 
Liliharibika mara kadhaa na kujengwa upya. Mwaka 262 BK liliharibiwa kabisa wakati wa uvamizi wa Wagodoni. Leo hii kuna nguzo moja tu inayoonekana.
 
AJABU LA 4: Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)

Sanamu ya Zeus mjini Olympia ilimwonyesha mungu mkuu wa dini ya Ugiriki ya Kale. Zeus aliaminiwa kuwa baba wa miungu wa Ugiriki.
 
Sanamu yenye kimo cha mita 12 ilimwonyesha mungu huyu akikalia kitini kama mzee mwenye hekima
 
Ilitengenezwa na mchongaji mashuhuru Phidias aliyejenga kiini cha ubao na chuma pamoja na jasi na kuifunika kwa ubao, dhahabu na pembe.
 
Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.
 
Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.
 
Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.
 
Lakini wakati wa karne ya 4 ilipelekwa Konstantinopoli ikasimamishwa pale hadi mwaka 475 ilipoharibiwa katika moto kubwa.
 
AJABU LA 6: Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)

Sanamu ya Kolossos kwenye kisiwa cha Rhodos ilikuwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale.
 
Kolossos ilikuwa mnara wa taa mwenye umbo la sanamu ya mtu aliyesimama kwenye mlango wa bandari na kushika moto kama mwenge. Kazi ya sanamu ilikuwa kuelekeza meli bandarini wakati wa usiku. Sanamu ilimwonyesha mungu wa jua Helios.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…