Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, yuko tayari kurejea katika Inter Milan kwa gharama ya mkopo wa £8.5m pamoja na marupurupu aliyokubaliwabaina ya klabu hizo. (Mail)
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kufanya dai jipya kwa ajili ya kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 Frenkie de Jong. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, yuko katika orordha ya Manchester United ya wachezaji inayoweza kusaini mkataba nao iwapo watashindwa kusaini mkataba na De Jong. (Fabrizio Romano, via givemesport)
Meneja wa Uholanzi na meneja wa zamani wa Manchester United boss Louis van Gaal alihusika kwa sehemu katika kumzuwia mlinzi wa Ajax Mholanzi Jurrien Timber, 21, kuhamia Old Trafford. (Marcel van der Kraan, Sky Sports)
Ajax wametenga euro milioni 40 (£34.3m) wanazotaka kuzitoza Sebastien Haller, huku Borussia Dortmund wakiwa na nia na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27- kutoka Ivory Coast. (90min)
Sunderland, Huddersfield na Bristol City wameweka dau la nyongeza la have £1m kwa ajili ya kiungo wa kati Muingereza mwenye umri wa miaka 21 anayechezea klabu ya AFC Wimbledon Jack Rudoni. (Sun)
Real Madrid tayari wanapanga kuanzisha kipengele cha kutolewa cha euro 150m (£128m) katika kandarasi ya mshambuliaji mpya wa Norway aliyenunuliwa na Manchester City Erling Haaland mnamo 2024. (AS)
Manchester United wana matumaini kwamba Barcelona watapunguza bei yao ya £80m kumuuza kiungo waUholanzi wa miaka 25- Frenkie de Jong kwa £10-15m. (Athletic, usajali unahitajika)
Kocha wa United Erik ten Hag amewaambia wakuu wa klabu hiyo kumsajili De Jong na kiungo wa kati wa Uswidi Christian Eriksen, 30, kwani watakuwa sehemu muhimu ya timu yake. (Mirror)
Mlinzi wa Manchester United Phil Jones, 30, iyuko kwenye orodha ya wachezaji wanaosakwa na Leeds United, lakini Whites huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Southampton na Fulham ambao pia wanamtaka Muingereza huyo. (Marca - usalili . unahitajika)
Liverpool wanajiandaa kumpoteza mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 30, kwa uhamisho wa bure msimu ujao wa joto baada ya kukataa kutimiza matakwa ya mkataba wake wa pauni 400,000 kwa wiki. (Mirror)
Manchester City wako tayari kumruhusu mchezaji wa matumizi Oleksandr Zinchenko, 25, kuondoka katika klabu hiyo - huku Everton ikiripotiwa kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine- huku City wakiandaa ofa ya kumnunua beki wa kushoto wa Brighton Mhispania Marc Cucurella, 23. (Fabrizio Romano)
Brighton wanatarajia kupokea takriban pauni milioni 50 kwa Cucurella, jambo ambalo linaweza kuwalazimu City kujitenga na mkataba huo. (Athletic, usajili unahitajika)
Liverpool wamemwambia mlinzi Neco Williams, 21, kwamba anaweza kwenda kwa mkopo msimu ujao, huku Nottingham Forest ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. (Mirror)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.