Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Barcelona wanataka kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde, lakini hawataki kulipa euro milioni 60 za Sevilla (£51.5m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Marca)
 
Brentford haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Denmark Christian Eriksen, ambaye alijiunga nao kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita. Manchester United pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30(90 Min)
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikaa msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest na kuwasaidia kupandishwa daraja hadi Ligi ya Premia. (Sky Sports)
 
Borussia Dortmund, ambayo ilimuuza mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 21 kwa Manchester City, inatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast Sebastien Haller kutoka Ajax kwa euro 36m (£31m). (ESPN)
 
Wolves wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Brazil Gabriel Barbosa, 25, kutoka Flamengo na kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, 21, kutoka River Plate. . (90 Min)
 
Rangers wanaweza kumuuza mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos ikiwa hawatakubali mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto 2023. (90 Min)
 
Manchester United wanatarajia fowadi wa Ufaransa Anthony Martial kuwa katika klabu hiyo msimu ujao kwa sababu ya kutovutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Manchester Evening News)
 
Manchester United wanamfikiria mlinda mlango wa Watford na Austria Daniel Bachmann kama msaidizi wa mchezaji wa kimataifa wa Uhispania David de Gea, 31, huku Mwingereza Dean Henderson, 25, akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford na kujiunga na Nottingham Forest. mkopo (Goal)
 
West Ham wanatazamiwa kutoa takriban pauni milioni 30 kwa mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 20, ambaye alicheza kwa mkopo Southampton msimu uliopita. (Sky Sports)
 
Tottenham waliwasiliana na kambi ya mchezaji wa Denmark Christian Eriksen wiki chache zilizopita lakini hawajafuatilia nia ya mchezaji wao wa zamani mwenye umri wa miaka 30, ambaye alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita huko Brentford. Football London)
 
Back
Top Bottom