Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vinasaidia pia kwenye kutibu homa, pumu, maambukizi ya bakteria, matatizo yanayo ambatana na mfumo wa upumuaji, angina, na matatizo ya kifua.
 
Vitunguu (Onions) ama kwa lugha ya kisayansi vinaitwa Allium cepa vipo kwenye kundi la mbogamboga, ambavyo vimekuwa vikitumika kwa upishi na kwenye tiba kwa maelfu ya miaka sasa.
 
Vitunguu vina kampaundi ambazo ni viondosha sumu vingi ambavyo vipo imara kwenye kuua sumu huru (free radicals) zinazopatikana kwenye mwili.
 
Vitunguu vimekuwa ni mimea yenye kutumika mara nyingi kwenye vyakula kwa zaidi ya miaka 7,000 , na katika muda huo mwingi vitunguu vilikuwa vinalimwa.
 
Bado kuna aina ya vitunguu pori kwenye baadhi ya maeneo ya bara la Asia, lakini kwa ujumla, kitunguu ni mmea unaokua na kulimwa dunia nzima.
 
Sifa ya vitunguu kupambana na bakteria ni pamoja na uwezo wa juu wa kuzuia matatizo yatokanayo na fangasi, tabia hiyo inavifanya kuwa ni tiba ya kwanza kwa kupunguza makali ya fangasi ukiwa nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…