Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata Shirika la kimataifa la afya duniani (WHO) limethibitisha kuwa vitunguu vinawanufaisha wale waliopungukiwa hamu ya kula na wale wanaosumbuliwa na atherosclerosis (kujirundika kwa cholesterol mbaya na vitu vingine ndani na nje ya mishipa ya damu, hali inayopelekea damu kupita kwa shida).
 
Wataalamu wa afya wanatujuza ukweli kwamba vitunguu hutoa mchango mkubwa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa pumu iliyokomaa, wenye allergy ya koo, na homa yenye kuambatana na kifua.
 
Vitunguu vina matumizi mengi yenye thamani kama tiba kwa sababu ya virutubisho, vitamini, madini, na kampaundi za asili zilizomo, zikiwemo kampaundi za sulfuric na quercetin pia.
 
Mbogamboga hizi pia zina madini kama vile calcium, magnesium, sodium, potassium, selenium, na phosphorus, na pia ni chanzo kizuri cha vitamini C, vitamini B6, na nyuzinyuzi (dietary fiber) pia.
 
Kwa Nini Nchini Nigeria mtu anapofariki wanachelewa sana Kumzika? Jana nilishare kuwa Muimbaji wa Gospel Osinach Nwanchuku amezikwa Juzi jumamosi na watu wengi kushangaa why wamechelewa kuzika? Nigeria ni Nchi ambayo Bado inaamini katika Mila na Desturi Zao. Ukiacha Masuala ya Kidini Maana ni Nchi ambayo ina waislamu wengi.Wao mtu akishafariki inafahamika wanazika mapema sana sababu ya Imani ya Kiislam. Wakristo wao huwa hawana haraka na ile imani ya kuwa Mtu akisha kufa huwa ameshakufa. Pia Wanaamini Marehemu anahitaji proper celebration ya kusherehekea maisha yake na wasipo Fanya hivyo Pengine anaweza kurudi kama mzimu kuwasumbua. . Pia Wao ni wengi na wamesambaa mataifa mbali mbali so wanapanga shughuli ambayo kila mmoja anataka kuwepo
 
Mwili wa marehemu unahifadhiwa watu wanaendelea na kazi na maisha yao ya kila siku na Ikifika siku ya kuzika ni shughuli haswaaa. Watu wanapendeza na Sare inakuwepo...Mwili unabebwa Na kuchezeshwa Kwa mbwembwe. . Muandishi wa Kitabu Cha ‘Things Fall Apart’ Chinua Achebe alifariki 21 March 2013 na kuzikwa Baada ya miezi 2..Alizikwa 23 May 2013 Yaani sherehe haswa yenye red carpet. . Mchungaji TB Joshua alipofariki alikaa mwezi mmoja ndio akazikwa..alifariki Tarehe 5 June 2021 Na kuzikwa Tarehe 9 July 2021 Mwanamuziki Tiea Savage alifiwa na Baba yake Tarehe 21 July na akazikwa 3 September 2021 Na Ilikuwa Bonge la Party
 
Back
Top Bottom