Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Virutubisho vilivyo ndani ya Zabibu ni Nishati, Wanga, Sukari, Kambakamba, Mafuta, Protini, Vitamini B1, B2, B3, B5, B6, B9,C, E na K, Madini, Kalsiamu, Chuma, Magnesium, Manganese, Sodiamu, Potasiamu, na Fosforasi.
 
Huimarisha mifupa

Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi kwenye zabibu, na madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya.
 
Kula zabibu mara kwa mara inasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri kuwa mkubwa. Pamoja na kuimarisha mifupa, madini haya husaidia mwili kufanya kazi vizuri.
 
Hulinda dhidi ya magonjwa ya moyo

Zabibu huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu na ina kampaundi za flavonoids ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Haya yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo na shinikizo la damu.
 
Kusafisha figo

Zabibu zina viondoa sumu ambazo husaidia kuondoa sumu kutoka kwenye figo. Pia hupunguza tindikali ya uric kwa kuongeza kiasi cha mkojo unaotengenezwa na figo.
 
Kupunguza lehemu

Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu kwenye damu. Zina kampaundi ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza unywonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo.
 
Machungwa hupunguza Shinikizo la damu.
Virutubisho (Phytonutrients) vitwavyo herperidin’s vipatikanavyo katika machungwa vinasaidia kupunguza shinikizo la damu.Pia tunda hili jamii ya citrus lina kiasi kikubwa cha folate ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kupata cardiovascular deseases(Magonjwa ya moyo).
 
Hupunguza Lehemu(Cholestrol) kwa kiasi kikubwa.
Limonin ambayo hupatikana katika machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza cholestrol katika mwili wa binaadamu.
 
Hupunguza Lehemu(Cholestrol) kwa kiasi kikubwa.
Limonin ambayo hupatikana katika machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza cholestrol katika mwili wa binaadamu.
 
Huzuia Magonjwa ya Figo.
Machungwa husaidia kuzuia mawe katika figo(Kidney Stones) na husaidia figo kuchuja sumu ziingiazo mwilini ipasavyo.Kunywa 1/2 mpaka Lita 1 ya juisi ya machungwa kwa siku itasaidia kupunguza kiasi cha pH katika mkojo kitu ambacho kitapunguza uwezekano wa kutengenezwa mawe(Kidney stones) katika figo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…