Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Raphinha, ambaye alijiunga na Leeds kutoka Rennes ya Ufaransa kwa £17m mwaka 2020, alicheza mechi 65 za Premier League katika klabu hiyo ya Yorkshire, akifunga mabao 17 na kutoa asisti 12.
 
Wakala wa Frenkie de Jong ameiambia Manchester United kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 25, yuko tayari kuondoka Barcelona lakini hataki kuhamia Old Trafford. (Sport - In Spanish)
 
Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo anatazamiwa kukataa ofa nono ya kujiunga na klabu moja ya Saudi Arabia, huku Bayern Munich na Atletico Madrid zikimhitaji mshambuliaji huyo wa Ureno, 37. (ESPN)
 
Juventus wamewasiliana na Arsenal kuhusu kumsajili mlinzi wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, kuchukua nafasi ya mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, ambaye anatarajiwa kujiunga na Bayern Munich. (Independent)
 
Mlinzi wa kulia wa wachezaji wa chini ya miaka 21 wa England Djed Spence, 21, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa muda mrefu kutoka Middlesbrough hadi Tottenham Hotspur na ada ya takriban £12m ikiwa imekubaliwa. (Times)
 
Barcelona wamehusishwa na kutaka kumnunua kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 19 Carney Chukwuemeka, 18, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa Aston Villa. (Mundo Deportivo)
 
Ikiwa watamleta Zinchenko au Gomez basi Nuno Tavares anaweza kuondoka, huku Marseille ikimtaka mlinzi huyo wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano, Twitter)
 
Back
Top Bottom