Mchezaji wa Middlesbrough mwenye umri wa miaka 21 amefanyiwa vipimo vya afya katika klabu hiyo ya Premier League kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 15. (Sky Sports)
Chelsea wanakaribia kumsajili kipa wa Chicago Fire wa Marekani Gabriel Slonina baada ya kuafikiana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. . (Fabrizio Romano)
Raphinha, ambaye alijiunga na Leeds kutoka Rennes ya Ufaransa kwa £17m mwaka 2020, alicheza mechi 65 za Premier League katika klabu hiyo ya Yorkshire, akifunga mabao 17 na kutoa asisti 12.
Wakala wa Frenkie de Jong ameiambia Manchester United kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 25, yuko tayari kuondoka Barcelona lakini hataki kuhamia Old Trafford. (Sport - In Spanish)
Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo anatazamiwa kukataa ofa nono ya kujiunga na klabu moja ya Saudi Arabia, huku Bayern Munich na Atletico Madrid zikimhitaji mshambuliaji huyo wa Ureno, 37. (ESPN)
Juventus wamewasiliana na Arsenal kuhusu kumsajili mlinzi wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, kuchukua nafasi ya mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, ambaye anatarajiwa kujiunga na Bayern Munich. (Independent)
Mlinzi wa kulia wa wachezaji wa chini ya miaka 21 wa England Djed Spence, 21, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa muda mrefu kutoka Middlesbrough hadi Tottenham Hotspur na ada ya takriban £12m ikiwa imekubaliwa. (Times)
Barcelona wamehusishwa na kutaka kumnunua kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 19 Carney Chukwuemeka, 18, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa Aston Villa. (Mundo Deportivo)
Ikiwa watamleta Zinchenko au Gomez basi Nuno Tavares anaweza kuondoka, huku Marseille ikimtaka mlinzi huyo wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano, Twitter)
Leeds United wanakaribia kuafikiana kuhusu mkataba wa euro 25m (£21m) na Paris St-Germain ili kumsajili mshambuliaji Mfaransa Arnaud Kalimuendo, 20. (90min).
Ajax wametoa ofa kwa mlinzi wa Rangers wa Nigeria Calvin Bassey, 22, huku klabu za Ligi ya Premia zikiwemo Brighton zikiwa na nia ya kutaka kumnunua. (Mail)