Nottingham Forest inatafuta dili la kumnunua mshambuliaji wa Nigeria Emmanuel Dennis, huku Watford wakitaka takriban pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)
Barcelona watafanya jaribio la mwisho kumsajili beki wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, licha ya kukiri kuwa hawawezi kufikia dau la Chelsea la pauni milioni 55 kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sport - in Spanish)
Borussia Dortmund wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 35, baada ya mkataba wake na Atletico Madrid kumalizika msimu huu. (Sky Sports - in German)
Chelsea wanatatizika kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua mlinda mlango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 27, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 26, kwa sababu ya madai yao ya mshahara
The Blues pia wanapata ugumu wa kuwaondoa wachezaji kama vile mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 28, na kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 28. (Telegraph -
Kiungo wa kati wa Aston Villa na England aliye chini ya umri wa miaka 19 Carney Chukwuemeka hana nia ya kusaini mkataba mpya Villa Park, huku Barcelona na Borussia Dortmund wakifuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Sky Sports)
West Ham ingependelea kumsajili mshambuliaji wa Blackburn na Chile Ben Brereton Diaz, 23, mbele ya winga wa Burnley Muingereza Dwight McNeil, 22. (Mail)
Brighton wanataka kumsajili kiungo wa Austria Florian Grillitsch, 26, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Hoffenheim kumalizika msimu huu wa joto. (Athletic - subscription required)
Mshambulizi wa Bordeaux na Korea Kusini Hwang Ui-jo, 29, anadai kuwa ana ofa ya kujiunga na West Ham msimu huu wa joto. (Sun) Newcastle inamfuatilia mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Slovenia Benjamin Sesko, 19(Mail)