Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong angeondoka tu Barcelona kwenda Chelsea lakini klabu hiyo ya London haiko tayari kulipa kiasi cha Manchester United kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport - in Spanish)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema hajui ni nani "aliyebuni" hadithi inayomhusisha mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo na timu ya Uhispania na kwamba "haiwezekani" mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 37 kujiunga nao. (El Partidazo de COPE, via Eurosport)
Juventus watamtazama mshambuliaji wa Werner na Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, kama hawataweza kukamilisha kumnasa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 29, kutoka Atletico Madrid. (Sky Sports)
Matumaini ya Tottenham kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 23, yanaweza kuathiriwa baada ya mchezaji mwenzake wa Juventus, Paul Pogba, wa Ufaransa, 29, kupata jeraha la goti. (Mail)
Chelsea wameelekeza mawazo yao katika kujaribu kumsajili beki Mholanzi Denzel Dumfries, 26, kutoka Inter Milan baada ya kutatizika kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Jules Kounde, 23, kutoka Sevilla. (Evening Standard)
Mkufunzi wa Barcelona Xavi anasema "haiwezekani" kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kwa sasa kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 yuko chini ya mkataba na Paris St-Germain lakini akaongeza kuwa "tutaona katika siku zijazo". (Goal)
Mlinda mlango wa Leicester City Kasper Schmeichel amekubali kujiunga na klabu ya Nice ya Ufaransa lakini uhamisho huo haujaidhinishwa kwani Foxes bado hawajapata mbadala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 35. (L'Equipe - in french)
Mwenyekiti wa Leicester City Aiyawatt Srivaddhanaprabha anasema klabu hiyo haikuwa na ofa yoyote kwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye mkataba wake na Foxes unamalizika msimu ujao wa joto. (Metro)
Southampton wamefanya uhamisho wa kuchelewa kujaribu kumsajili winga wa Manchester City Muingereza Sam Edozie, 19, ambaye alitarajiwa kujiunga na Bayer Leverkusen. (Mail)
Chelsea inazuia Barcelona kumnunua mlinzi wa Uhispania Marcos Alonso, 31, na Cesar Azpilicueta, 32, kutoka kwao kwa sababu ya uhamisho wa timu ya Uhispania kwa Kounde. (Sport - in Spanish)
Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anasafiri kurejea Uingereza na atafanya mazungumzo na Manchester United kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo. (Athletic - subscription required)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.