Wakati huu wanyama wote ambapo huliwa na mamba ndio wakati ambapo hulipiza kisasi, mfano kenge, mijusi wakubwa pamoja na ndege, humtegea anapopeleka watoto wa awamu ya kwanza wale wanaosaria hujeruhiwa vibaya, au kubebwa kama chakula na wanyonge wa Mamba, na mamba hujisikia tabu sana kiasi kwamba anapoibuka katika maji huwatizama kwa jicho la Shari sana.
Watoto wa Mamba ukiwaona katika udogo wao ni wanashangaza sana, hutokaa ufikirie kwamba ndio hao wafikapo ukubwani hufikia urefu wa futi 13 na zaidi, na uzito wa kilo zaidi ya 1000, ni viumbe ambao huonekana wadogo sana unaweza hisi labda ni kenge tuu.
Kwa taarifa yako Mamba ni miongoni mwa wanyama wakubwa sana duniani, meno yake yamejipanga kama msumeno, ana macho makubwa, ngozi ngumu na mkia mrefu ambao humsaidia katika kuwinda, hupendelea sana kukaa kwenye maji lakini jua lichomozapo na likalibiapo kuzama hupendelea sana kwenda kuchukua vitamin.
Ajabu la mnyama huyu ni moja, pamoja kwamba wanyama wanaokula nyama tuu ndio huishi muda mfupi, lakini yeye maisha yake ni marefu anaweza kugonga miaka 50 na zaidi kabisa
Chakula kikuu cha Mamba ni nyama tuu, hutafuna samaki, wanyama wadogo wadogo nk, hapo ni wakati umri ukiwa bado Mdogo, lakini umri unapoongezeka mnyama mamba moja ni nyumbu
hawa huwakamata kiurahisi kwa sababu ya ujinga, Twiga anapofata maji, mbogo, wakati mwingine hujaribu hata kumuwinda tembo lakini anapotokea mama wa tembo zoezi hill huishia hapo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.