Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyati hutumika kama kitoweo kwa wananchi nahivyo kujiongezea afya nzuri kwa kula protini itokanayo na nyama ya nyati.
 
Pia malighafi kama ngozi, kwato na pembe za nyati hutumika kutengenezea vitu kama viatu, nguo na mapambo mengi sana ya nyumbani na hata yakuvaa mwilini pia.
 
UHIFADHI HAPA NCHUNI KWETU TANZANIA

Ni jambo kidogo lakujivunia kuwa hadi sasa nyati bado hawajaingizwa katika kundi la wanyama wanaoelekea kutoweka duniani
 
Lakini hii haitoshi kujiridhisha na kuamini kwamba wataendelea kubaki idadi kama hii iliyopo kwa sasa kwasababu nyati wetu wanakumbwa na matatizo mengi sana huko hifadini.
 
CHANGAMOTO/MATATIZO YANAYO WAKUMBA NYATI HAPA KWETU TANZANIA

1.Ujangili ulio kithiri hasa katika hifadhi zetu za taifa. Nyati huwindwa sana na majangingili kwa dhumuni la nyama,

ngozi na malighafi zake nyingine. Hii hupelekea sana kupungua kwa kiasi kikubwa kwa wanyama hawa hifadhini.
 
Uharibifu wa mazingira hasa unaosababishwa na binaadamu katika maeneo tengefu ya wanyamapori. Mazingira yamekuwa yakiharibiwa sana na hatimae nyati pamoja na wanyama wengine kukosa chakula na kulazimika kuhama maeneo yale. Yote hii husababishwa na uvamizi wa maeneo ya uhifadhi kutokana na kuongezeka kwa shughuli za binaadamu.
 
Magonjwa mbali mbali kama kimeta na homa ya bonde la ufa, Japo magonjwa sio tatizo kubwa sana lakusema kwamba nilakutilia mkazo sana kwasababu wanyamapori wamezaliwa poroni wakiwa na vinasaba vya kuwasaidia kupambana na magonjwa mbalimbali tofauti na wanyama wafugwao. Wanyamapori wana uwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa hasa ukulinganisha na wanyama tunaowafuga majumbani kwetu.
 
SIASA katika uhifadhi, nadiriki kusema kuwa siasa ni sumu kubwa kama lilivyo tatizo la ujangingili katika wanyamapori. Viongozi wengi wamekuwa wakiingiza suala la siasa katika uhifdhi na hatimae kufanya shughuli za kihifadhi kuwa nguimu sana. Na yote hii hutokana na maslahi yakutaka kura toka kwa wananchi nakusahau kuwa kuna vizazi vinakuja ambavyo vitahitaji kuona uwepo wa nyati na wanyamapori wengine katika hifadhi zetu za taifa.
 
Uwindaji dhaifu, kuna tofauti kubwa sana tunaposema ujangili na uwindaji dhaifu. Uwindaji dhaifu ni kwamba mtu tayari anakuwa na kibali cha uwindaji na anapewa ruhusa yakuwinda nyati mmoja au wawili kutokana na kibali chake. Lakini anapokuwa kule anakiuka taratibu nakuzidisha idadi ya nyati aliotakiwa kuwinda. Pia maranyingi hutolewa vibali vya kuwinda nyati madume lakini mtu huwinda mpaka majike na watoto hii hupelekea sana kupungua kwa wanaya hawa hasa tu kutokana na uwindaji dhaifu.
 
Migogoro iliyopo baina ya wanyamapori na binaadamu, nyati niwanyama ambao huishi kwa kuhama na pale wanapohama kuna wakati hupita mashambani kwa watu nakula mazao yao, Hii hupelekea wanavijiji kuwauwa kwa sumu au hata kwa kuwachoma mishale. Lakini tukirudi nyuma hii husababishwa na watu kuvamia maeneo ya uhifadhi nakuanza shughuli za kibinaadamu maeneo hayo.
 
NINI KIFANYIKE KUWANUSURU NYATI WETU

1.Kupambana na ujangili kwa hali na mali kwa kuongeza askari wanyamapori katika maeneo tengefu ya uhifadhi wanyamapori na hifadhi za taifa. Hii pia inafatana na kuongeza doria za mara kwa mara katika maeneo husika ili kupunguza adha ya ujangili hapa nchini.
 
Migogoro iliyopo baina ya wanyamapori na binaadamu, nyati niwanyama ambao huishi kwa kuhama na pale wanapohama kuna wakati hupita mashambani kwa watu nakula mazao yao, Hii hupelekea wanavijiji kuwauwa kwa sumu au hata kwa kuwachoma mishale. Lakini tukirudi nyuma hii husababishwa na watu kuvamia maeneo ya uhifadhi nakuanza shughuli za kibinaadamu maeneo hayo.
 
NINI KIFANYIKE KUWANUSURU NYATI WETU

1.Kupambana na ujangili kwa hali na mali kwa kuongeza askari wanyamapori katika maeneo tengefu ya uhifadhi wanyamapori na hifadhi za taifa. Hii pia inafatana na kuongeza doria za mara kwa mara katika maeneo husika ili kupunguza adha ya ujangili hapa nchini.
 
Kuwepo kwa sera ambazo zitasaidia kupambana na uharibifu wa mazingira hasa karibu na hata ndani ya maeneo ya uhifadhi ili ili kupunguza kuhama hama kwa wanyama hawa kwa ajili yakutafuta chakula.
 
Kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wakuwatunza wanyamapori na utunzaji wa mazingira kwasababu watakuwa mabalozi wazuri hata kuweza kuwafichua majangili ambao wanaishi katika maeneo yao.
 
Kuwaanzishia wana vijiji miradi mbali mbali ili wawe wanatumia muda mwingi kuwaza maendeleo ya miradi yao na si kuwinda wanyama pori. Shukrani sana kwa shirika la Uhifadhi wa mazingira kwa wanyamapori na maendeleo ya jamii (ECOWICE-Environmental Conservation for Wildlife and Community Enterprise) kwa miradi yao wanayo iendesha kama uoteshaji wa uyoga unasaidia sana kwa kiasi kikubwa katika utunzaji wa mazingira na uhifadhi wanyamapori.
 
Ufatiliaji mzuri na uhakiki wa vibali vya uwindaji vinavyo tolewa kwa wawindaji ili kuepuka changamoto ya kuwindwa kwa wanyama zaidi ya idadi ya waliotakiwa kuwindwa. Bali pia kuwafatilia wahusika pale wanapokuwa wanatekeleza shughuli ya uwindaji ili pasiwepo na utofauti wowote kati ya kibali kisemavyo na kile kinacho fanyika eneo la uwindaji.
 
Migogoro baina ya binadamu na wanyamapori itafutiwe ufumbuzi haraka kwasababu hii pia inazidi kukua siku baada ya siku. Mfano kupaka pilipili maeneo ya mazao au pembezoni mwa mashamba hii husaidia sana kuzuiya nyati na wanyama wengine walao mazao wasisogee karibu kutokana na kuwasha kwa pilipili.
 
Kupambana sana na kuitokomeza SIASA katika suala zima la uhifadhi wnyamapori mana ni sumu inayoenea polepole na mwisho wake kusababisha upotevu wa wanyamapori. Panapo hitajika ukweli basi pasemwe nah ii hasa wanayo WABUNGE kwani wamekuwa waleta porojo sana linapokuja suala lakkuwataka watu kuhama maeneo ya uhifadhi. Wamekuwa wakitetea sana suala hili kwa maslahi yakutaka kupigiwa kura msimu wa uchaguzi unaofuata bila kujali maslahi na thamani ya wanyamapori kwa watanania wote.
 
Kutekelezwa kwa shera zilizowekwa ambazo zinasimamia masuala ya maliasili bali pia na usimamizi wa wanyamapori. Sheria hizi zifanye kazi bila kuangalia alieye kiuka shria ni nani na ana wadhifa gani. Kwani tukumbuke ukimuangalia mtu cheo alichonacho na kuharibu mali ya uma anaumiza wananchi walio wengi sana.Hivyo mamlaka husika ziwe macho na kufatilia utekelezaji wa sheria hizi.
 
Back
Top Bottom