Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kisiwa cha Pemba; kisiwa hichi kiko umbali wa 55km kutoka Tanzania bara na kutunza spishi nne za kipekee ambazo ni Pemba green pigeon, Pemba scops owl, Pemba sunbird na Pemba white-eye.
 
Fukwe za jiji la Dar es salaam: fukwe hizi ambazo zimeundwa na tambalale ya tope la mawimbi ya bahari, pia kama kiunganishi cha maji ya chumvi na baridi kutoka vijito tofauti vya jiji pamoja na misitu ya mikoo hivyo kutoa nafasi kubwa kwa makazi tofauti ya ndege ambapo inajumuisha spishi 450.
 
Pia fukwe hizi muhimu kwa ndege wa masafa miongoni mwao ni waders kama Grey plover, little stint na curlew sandpiper.
 
Hifadhi ya taifa Ruaha: ni miongoni mwa hifadhi kavu nchini ambayo ina jumla ya spishi 560 za ndege, ambapo kati ya hizo spishi mbili hupatikana Tanzania tu ambazo ni Ashy starling na yellow-collared lovebird.
 
Hifadhi ya taifa Serengeti: hifadhi yenye jina kubwa nchini na imeweza pokea tuzo nyingi za kimataifa kama sehemu pekee bora barani Afrika kwa utalii, ikiongezewa sifa na nyumbu wenye misafa ya msimu Tanzania na Kenya
 
Inapatikana katikati ya ziwa Victoria na bonde la ufa la mashariki karibu na hifadhi ya Masai Mara Kenya na upande mwingine inapakana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
 
Serengeti ina spishi kuu tatu za kipekee ambazo ni Grey-breasted spurfowl, Fischer’s lovebird na Rufous-tailed weaver pia ndege wa masafa marefu kutoka magharibi na ulaya ni rahisi kuwaona katika kipindi chao cha safari.
 
Eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro: hili limeorodheshwa kuwa na jumla ya spishi 500 za ndege ikiwa na makundi makubwa ya Fischer’s lovebirds, pia eneo hili lina mabwawa na ardhi owevu ambayo ni muhimu kwa greater and lesser flamingos, pia rahisi kumuona faru mweusi mnyama ambaye yupo hatarini zaidi kutoweka.
 
Hifadhi ya taifa Mkomazi: hifadhi hii inapakana na safu za mlima wa Pare kusini, na ina ndege tofauti kama Friedmann’s lark, pygmy batis, three-streaked Tchagra, shelley’s starling na Pringle’s Puffback.
 
Hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa: hifadhi hii ipo upande wa kusini magharibi kutoka jiji la Dar es salaam ambako kuna msitu wa akiba wenye spishi mbali mbali na mara chache kuonekana maeneo ya kawaida ambazo ni Udzungwa partridge, Dappled mountain-robin, Sharpe’s akalat, Olive-flanked robin-chat pamoja na White-chested alethe.
 
Safu za milima ya Uluguru: ni eneo ambalo lipo kati kati ya jiji la Dar es salaam na Udzungwa, ndo eneo pekee kwa ajili ya Uluguru bush-shrike na Loveridge’s sunbird pamoja na spishi nyingine tano, na mara nyingine inaweza ikatokea bahati kumuona Abbott’s duiker ambaye ni mnyama jamii ya swala na hupatikana kwa nadra sanaaa nchini.
 
Safu za milima ya Usambara mashariki: eneo hili ni miongoni mwa maenao muhimu Afrika bala kwa uhifadhi wa spishi zinazosumbuliwa na zenye tishio la kutoweka kidunia. Spishi hizo ni kama Usambara eagle owl, Sokoke scops owl, Long-billed tailorbird, Dappled mountain-robin, Swynnerston’s robin pamoja na Usambara weaver.
 
Misitu ya fukwe za wilaya ya Lindi: fukwe hizi ni eneo muhimu kwa spishi nyingi za ndege wa misitu ya fukwe kama Southern banded snake eagle, East coast akalat, Spotted ground-thrush pamoja na Livingstone’s flycatcher.
 
Pamoja na kwamba nchi yetu ina maeneo mengi na jamii nyingi za ndege, bado kuna changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinarudisha nyuma uhifadhi wa ndege kiduniana na kitaifa pia
 
Back
Top Bottom