Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jua huwa linatoa cheche ambazo muda mwingine huwa zinafika karibu na anga la dunia. Mara ya mwisho cheche ya jua kukaribia duniani ilikuwa tarehe 3 Septemba 2012 ambapo iliikosa duniani kwa karibu sana. Wanasayansi wa anga wanatabiri kuwa kuna cheche nyingine itatokea kufikia mwaka 2022 yenye ukubwa sawa na ile ya 2012.
(Wikipedia/SolarFlare)
 
Mwaka 2012 Choi Gap Bok alitoroka gerezani kwa kupitia katika tundu la kupitishia chakula kwa wafungwa. Tundu lilikuwa na urefu wa 5.9 inch na upana 17.7 inch. Choi' alikuwa ni mzoefu wa kufanya Yoga, alijipaka mafuta kisha kuanza kujikunja mpaka kupita. Wakati anafanya hayo walinzi walikuwa wamepitiwa na usingizi.
 
Pombe unapokunywa huingia moja moja kwenye damu kwa matumizi ya mwili ndiyo maana unapata matokeo yake kwa haraka. Maji unapokunywa hupitia mchakato wote wa mmeng'enyo (Kufyonzwa) kwaajili ya matumizi katika mwili.
 
Mwaka 1958 bomu la nyuklia lenye uzito wa kg 3,400 lilipotea karibu na kisiwa cha Tybee huko Georgia, Marekani katika ajali wakati wa mazoezi ya Jeshi la anga la Marekani. Mpaka sasa halijapatikana.
 
Apple inasemekana wana kitengo cha siri cha usalama kwaajili ya kuwachunguza wafanyakazi kuhakikisha hakuna anaevujisha siri ya kampuni. Na hiyo ni mojawapo ya sababu ya kuwa na nafasi kubwa kuchaguliwa Chuo Kikuu Cha Havard' kuliko kuajiriwa na Apple'
 
Unywaji wa soda yenye kiasi cha 600 ml kila siku inazeesha uwezo wa seli za damu kwa kiwango sawa na mvutaji wa sigara wa miaka 4 mpaka 6. Kama ni mtumiaji mkubwa wa soda hakikisha unapenda kunywa maji mengi pamoja na mazoezi.
 
Wanaotumia mkono wa kushoto huwa na uwezo wa kufanya maamuzi kwa haraka zaidi tofauti na wanaotumia mkono wa kulia, sababu ubongo wao una uwezo wa kusafirisha taarifa kwa haraka zaidi kwa pande zote mbili kushoto na kulia.
 
Thomas de Mahy, alikuwa anaunga mkono utawala wa Ufaransa uliotolewa madarakani kwa mapinduzi karne ya 18. Baada ya mapinduzi alihukumiwa kunyongwa. Alipopewa karatasi ya hukumu asaini, alisoma kisha akamwambia hakimu "Kuna maneno matatu mmekosea kuandika". (Wikipedia & VintangeNews)
 
Amado Carrillo Fuentes maarufu kama "Lord of the Skies" alipewa jina hilo sababu alikuwa anamiliki Ndege tofauti 727 alizokuwa anatumia kusafirisha madawa ya kulevya. Alikuwa akifanya Upasuaji mara kwa mara kujibadilisha viungo mbalimbali kama sura ili kuwakwepa polisi. Alifariki mwaka 1997 sababu ikiwa kuzidisha sana Upasuaji wa mwili wake
 
Anold Schwazeneiger' kwa kila neno aliloongea katika filamu ya Terminator 2 alilipwa Tsh Milioni 49. Aliongea maneno 700 Jumla akalipwa Tsh Bilioni 34. Maneno "Hasta la vista, baby" aliyotamka alilipwa Tsh Milioni 197.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…