Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia, mbwa mwitu wenye njaa walivamia makambi ya wanajeshi wa Urusi na Ujerumani na kuanza kuwala. Ilibidi wanajeshi hao (ambao walikuwa maadui) waungane kwa muda kupambana na mbwa mwitu kwanza.(War History)
 
Angelina Jolie alikodi mtu wa kumuua baada ya kuzidiwa na msongo wa mawazo. Muuaji huyo alikubali lakini akamwambia asubiri kwa mwezi ndo atamuua. Lengo la muuaji lilikuwa kumpa muda Angelina Jolie abadilishe mawazo, alifanikiwa. (IMDbNews
 
Ulaji mara kwa mara wa Vitunguu Saumu' husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa' kwa wanaume. Husaidia kulainisha mafuta yote yanayopatikana katika mishipa ya damu hivyo huongeza kasi ya mzunguko wa damu kwa haraka. Wakati wa tendo la ndoa damu huteremka kwa urahisi mpaka kwenye Uume' na kuzidi kuongeza hamu zaidi
 
Conrad Henri Roy III, alijiua akiwa na miaka 18 mwaka 2014 baada ya kushawishiwa na mpnz wake, Michelle Carter. Conrad na Michelle walikuwa wanasumbuliwa na msongo wa mawazo ambapo Conrad alikuwa anataka kujiua lakini anashindwa. Michelle alianza kumshawishi ajiue ili aachane na matatizo ya duniani. Hatimaye Conrad alijiua tarehe 13 July 2014 kwa gesi ya kabonimonoksaidi ndani ya gari lake. Michelle alishtakiwa na akafungwa lakini baadae aliachiwa kwa utetezi wa kuwa alifanya makosa akiwa na matatizo ya akili.(Rolling Stones, Wikipedia, Quora)
 
Wafungwa nchini Ujerumani wanaruhusiwa kupika vyakula vyao, kuunda timu zao za mpira, kupamba vyumba vyao wanavyotaka, kucheza magemu, kuvaa nguo za kawaida, kutembelewa na wenza wao kwaajili ya huduma ya kimwili na kumiliki funguo za vyumba vyao. Wafungwa wanaonesha tabia nzuri zaidi huruhusiwa kwenda kutafuta kazi mtaani pia wanapewa ruhusa ya kutoka kwaajili ya matembezi ya mara kwa mara. Lakini kumbuka unaruhusiwa pia kutoroka sababu ni haki yako ila usiharibu mali yoyote ya gereza.
 
Kuna muda Brazil hunyesha mvua ya Bui bui. Mwaka 2014 Sri-Lanka ilinyesha mvua ya samaki. Mwaka 2009 Ishikawa,Japan ilinyesha mvua ya Vyura. Sababu inasemekana ni kimbunga kidogo ambacho huchota viumbe hao na kuwatupa mbali kama mvua hivyo kuonekana kama wanatokea katika mvua.
 
Furaha yako sio furaha yake. Jifunze kujipa furaha mwenyewe mwambie nae ajifunze kujipa furaha kwanza kisha mkutane wote kwa pamoja ili mfurahi. Usimpe mwenzako wajibu wa kukupa wewe furaha wakati wewe mwenyewe kujipa furaha umeshindwa huo ni Ubinafsi", Will Smith
 
Furaha yako sio furaha yake. Jifunze kujipa furaha mwenyewe mwambie nae ajifunze kujipa furaha kwanza kisha mkutane wote kwa pamoja ili mfurahi. Usimpe mwenzako wajibu wa kukupa wewe furaha wakati wewe mwenyewe kujipa furaha umeshindwa huo ni Ubinafsi", Will Smith
 
IMG_0844.jpg
 
Back
Top Bottom