Serikali ya Uholanzi imeidhinisha mipango ya kuruhusu kifo cha mapema au mauaji ya huruma kwa watoto wenye ugonjwa usiopona kati ya mwaka 1 na miaka 12.
Alisema utafiti uliofanywa na wataalamu ulionesha umuhimu wa kubadilishwa kwa sheria hiyo.
"Utafiti ulionesha kuna umuhimu wa maisha kukatizwa miongoni mwa madaktari na wazazi wa watoto wanaougua magonjwa yasio na tiba, ambao wanapata tabu bila usaidizi wowote na hatimaye watakufa tu siku zijazo," Bwana de Jonge alisema katika barua aliyoiwasilisha bungeni.