Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha sio tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla
 
Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara.
 
Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha, usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine
 
Hakikisha jina la biashara yako linamvuto na kukubalika katika jamii husika. Pia Jihusishe na watu mbalimbali walioendelea katika ujasiliamali ili uweze kupata mawazo mbalimbali na mbinu mpya za kuweza kufanikiwa katika ujasiliamali.
 
Tafuta kitu kitakachokuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa wakati huo katika eneo husika, ukitumie kama njia ya kujitangaza. ukifanikiwa katika hilo basi utajijengea channel kubwa na watu wengi watakujua na hiyo itakurahisishia safari ya kufahamika kwa biashara yako.
 
Fanya utafiti sokoni kujua watu wanazichulia vipi bidhaa au huduma unayotaka kutoa ili kuweza kujua wapi unakosea na kujirekebisha mapema iwezekanavyo ili kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri na watu.
 
Kama unataka kufanya biashara na huduma ambayo kuna wengine wanafanya, hakikisha biashara yako iwe na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na watu wengine, na ujue wanakosea wapi na utafanya nini cha tofauti la sivyo utakuwa nyuma yao milele kwani kinachowavuta watu kuja kununa kwako ni utofauti kati yako na wapinzani wako na sio tu kwa kuwa bidhaa unayo
 
1737891975782.jpg
 
Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe

Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake, na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote.
 
Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako!
 
Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya yaliyopita

Kuhisi kwa kuwa kuna kitu Fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basimaishahayatawezekana tena. Pengine ulifiwa, kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au kufilisika.
 
Kukubali kuzungukwa na watu wasiokufaa

Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali kushindwa, huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu nao watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa tayari kupiga hatua zaidi.
 
Kukimbia matatizo na kuogopa kushindwaJe wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila tunapoanguka. Na epuka Kuhisi kuna mtu mwingine anahusika na furaha yako.
 
Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe

Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu, kuiba, kuua nk!
 
Kuamini Wewe ni Mifupa na nyama tu!Hili ni kosa kubwa sana maishani, wengi huamini binadamu n mifupa na nyama tu, hivyo hakuna hata ya kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa tu “eti” Mwisho wa siku tutakufa na kuzikwa! Je, Unawaachia nini wanao na kizazi chako? Je kwa nini hasa Mungu alitupa utashi tofauti na Mbuzi na wanyama wengine?
 
Kumbuka, Tungeamua kuamini kuwa sisi ni Nyama na mifupa tu, kusingekuwa na Magari, Simu, Majengo ya kisasa, na Hata hii dini tuliyonayo tusingeipata.“do your part, make world a better place
 
Back
Top Bottom