Tatizo kubwa la mazoea ni namna yanavyoleta mabadiliko madogo madogo, saa nyingine hayaonekani kwa macho, yanakuja kwa mwendo wa kinyonga, mdogo mdogo, hatua kwa hatua. Ukitaka kuona matokeo kwa haraka utakosa subira, utaruka hatua muhimu, utaishia kuharibu mchakato au utaachia njiani.