Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Na ndio ndege ambae unaweza ukamfundisha
matendo hata lugha na akaielewa zaidi ya
Kasuku ndomana zamani alikuwa anatumika
kama mjumbe, mfano,Kupeleka ujumbe wa
maandishi sehemu fulani.
 
Ndege ni miongoni mwa viumbe ambao
wametawanyika sehemu nyingi duniani. Katika
makala ya leo tutamjua ndege mmoja ambaye
ni mvivu wa kuatamia na kulea vifaranga
vyake.
 
Kekeo ndege ambao wanapatikana maeneo
mbalimbali hapa duniani ni wasiri sana lakini
kama nilivo dokeza kidogo hapo juu ndege
hawa huonekana kuwa na asili ya uvivu hasa
katika kuatamia mayai na kulea vifaranga
vyao.
 
Hivyo katika makala ya leo nitamzungumzia
kekeo anae patikana barani Afrika tu na si
kwingineko duniani huku na sisi hapa nchini
Tanzania tukijivunia uwepo wa ndege huyu.
 
Kichwani, mabawa na sehemu ya juu ya miili ya
ndege hawa wana rangi ya kijivu iliyo kolea
zaidi huku shingoni na kifuani wana rangi ya
kijivu iliyo pauka.
 
Wana mabawa marefu na mikia mirefu yenye
rangi ya kijivu iliyokolea na rangi nyeupe
kwenye ncha ya mikia yao
Madume wana macho yenye rangi ya njano
huku majike wakiwa na macho yenye rangi ya
kahawia inayo ng’aa zaidi.
 
Wana midomo yenye rangi ya njano hasa
sehemu ya shina na kuwafanya karibu nusu ya
midomo yao kuwa na rangi ya njano huku
sehemu ya ncha ikiwa na rangi nyeusi.
 
Rangi ya njano katika midomo ya kekeo kijivu
huwafanya watu wengi kuwachanganya na
kekeo wa kawaida kwani hata wao pia wana
midomo yenye rangi ya njano.
 
Back
Top Bottom