Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jike hutaga mayai kwenye viota vya ndege
wengine na anapo kuta kiota kina mayai basi
huyatoa kisha kutaga mayai yake na kuyaacha
yaatamiwe na ndege mwenye kiota.
 
Sauti ya dume hutoka kwa mlio wa “koo-koo-koo” ambao huwa na mfumo wa sauti ya piliila yenye kusikika zaidi huku sauti ya jikehusikika kwa mlio wa ”kwik-kwik-kwik”.
 
JE, WAJUA?

Baadhi ya jamii huamini kwenye sauti au milioya kekeo? Baadhi ya jamii hapa nchini Tanzania huaminikatika sauti au milio ya baadhi ya jamii zakekeo hasa kwenye suala la misimu ya mvua.
 
KUZALIANA

Unapofika msimu wa kuzaliana dume na jike
kwa pamoja hulia milio ya kuashiria tukio la
kupandana na dume ndio huwa ni mtawala wa
himaya.
 
Jike anapo karibia kutaga basi hutafuta kiota
cha ndege mwingine mwenye mayai na kisha
kuyatoa mayai ya ndege yule nje ya kiota na
kutaga mayai yake.
 
Mara nyingi hupendelea kutaga kwenye kiota
ambacho mayai ya ndege huyo mwenye kiota
yanafanana na mayai yake ili ndege mwenye
kiota asiweze kugundua mayai hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…