Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia ya kutaka kuonekana mkamilifu ndio chanzo cha wewe kukosa furaha. Kila ukikosea hata kidogo unaumia na kuwaza siku nzima. Hata jambo dogo na jepesi inatumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kulifanya bila kukosea, hapa ndio msongo wa mawazo unapoanzia.

No one is perfect
 
Ukienda msibani ndio inakujia ile hisia kuwa wewe sio kitu bali ni mavumbi tu.
 
1758477251933.jpg
 
KUWA NA KIASI
Kuwa mwema lakini usikubali kufanywa mjinga

Penda lakini usikubali kutumika tu.

Amini watu lakini usikubali kudanganywa

Ridhika lakini usichoke kutafuta.

Kila kitu kwa kiasi.
 
Usimwamini mbwa mwenye njaa anakuaga na tabia ya kumfuata kila mwenye chakula.
 
Kuwa makini sana na watu wanaokuja kwenye maisha yako. Wale unaowachukulia poa mara nyingi huwa ni baraka ambayo imejificha na upendo wao huwezi kuupata kwa wengine.
 
Unapopanga mipango ya maisha usihusishe umri wako. Halafu panga kama vile utaishi maisha marefu.
 
Kama unataka kufanikiwa ni lazima matendo yako yaendane na malengo yako. Kwa mfano unataka ku-save pesa ni lazima uache matumizi yasiyo lazima.
 
Ukishapata unachoomba omba nidhamu ya kukitunza na busara za kukifanya kiwe bora zaidi.
 
Kila mtu alikua na bado anayo ndoto ya kuishi maisha mazuri. Kama wewe umepata usijione una akili sana au wewe ni mtu special. Ni suala la muda tu na wengine milango itagunguka
 
Umeshapenda sana, umeshasaidia sana, umeshahurumia sana umeshawasifia sana umeshawajali sana

Ni.muda sasa wa wewe kufanya hayo yote kwa ajili yako. Unastahili yote.
 
Back
Top Bottom