Usiwe na kiherehere cha kusaidia kila mtu wengine wapo kwenye kipindi cha MALIPO DUNIANI wanalipa ubaya ambao waliwafanyia wengine. Acha ulimwengu uchukue nafasi yake kwa kuwalipa kutokana na matendo yao.
.
Shetani hajawahi kuwa mbaya, siku zote ni mzuri anavutia ni mtamu na ni raha sana ukiwa, mpaka pale anapokua chanzo cha maumivu yako ndio unaanza kumlaumu na kumuona hafai.
Fanya tathmini ya siku ya leo. Wapi umekosea na kwanini, pale ulipofanya vizuri hata kama ni kidogo jipongeze. Lala ukiwa na amani kuwa kuna kitu umefanya leo.
Kwenye maisha silaha kubwa ya pekee uliyonayo ni afya ya akili. Usipokuwa imara kichwani hamna ambacho utaweza kukifanya kwa ufanisi. Linda Afya yako ya akili.
Kila mtu ameumbwa kwa uwezo wake na kwa jinsi Mungu alivyoona inafaa. Kubali uwezo ulionao na uutumie kupata k8le unachotaka. Maisha bora sio uwe elimu na elimu sio lazima uipate darasani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.