Kamwe usitake kujua watu wanavyoelewa kwa sababu watu huwa wanaelewa wanavyoelewa''. Hivyo usitake kueleweka na watu jinsi wewe unavyotaka kueleweka, kimsingi ni sawa na ukiwa darasani jibu la 2x3 ni sawa na jibu la 3x2.
hakuna ujinga mkubwa kama kumdanganya anayekuamini na kumuamini anayekudanganya. Hii ni sawa na kuujua ukweli halafu ukaamua kuuamini uongo. Huyu ni kama wewe basi JITATHIMINI halafu ubadilike kwani itakuwa ndio mtego wako wa kukuzuia KUYAISHI MALENGO YAKO!
Maisha hayataki uwe mtu wa kuchukulia mambo serious kila wakati. Wakati mwingine yaulize MATATIZO yako maswali magumu. Usiwe mtu wa kutingishwa tingishwa na maoni ya watu kuhusu maisha yako.
Hatutaishi MILELE hapa duniani! Kikubwa hakikisha kuwa unafanyika baraka katika maisha ya watu wengine ukiwa bado kwenye huo mwili. Kwani siku inakuja, utauacha huo mwili lakini kama uliwagusa watu basi utaendelea kuacha ALAMA ISIYOFUTIKA kwenye maisha yao.
Ukikubali kuishi maisha yasiyo na maono ni kukubali kuishi kama kunguru! Utataka kuwa kila mtu; utataka ueleweke na kila mtu; utataka kudandia na kushindana na maono ya wenzako na mwisho wa siku utajikuta UMEFARIKI badala ya KUFA.
Mafanikio yana tafasiri tofauti kwa watu tofauti, itafute ile tafasiri ya kwako kuhusu mafanikio halafu ifanyie kazi. Haijalishi unaonekana umechelewa kiasi gani, endelea kuamini katika hiyo ndoto yako. Usiache kufanya hata kama unaona matokeo yanachelewa!
kama huwezi kutumia kinywa chako kuwatia moyo na kuwabariki watu basi usikitumie kuwakatisha tamaa. Mungu hapendi na atakupiga tu. Ukiweza kujifunza KUONGEA KIDOGO tena pale panapobidi utakuwa UMEJIEPUSHA na VITA VINGI katika maisha yako.
hekima unayopaswa kuijua ni kuwa sio kila ukweli ni mzuri na wa kusemwa, chagua vyema vya kusema kwa kuunganisha ubongo wako na akili yako! Halafu yule unayemuona HAFAI na ananuka kama kinyesi sisi wengine tunamuona ni MBOLEA bora ya kurutubisha ardhi iliyochoka.
Nakukumbusha kuwa ukimfanya Mungu wa dharula na yeye atakufanya wa dharula! Unapoacha kuomba, unaanza kuwa na tabia mbaya ya KULALAMIKA LALAMIKA. Usiwe vugu vugu kwa kumtafuta Mungu wakati wa SHIDA tu, shida zitakuwepo wakati wote kwenye maisha yetu.
huu ULIMWENGU tunaoishi una SIRI nyingi sana ambazo zimefichwa kwa watu wengi na kuruhusiwa kwa wachache sana kuzifahamu ili kuwatawala vyema hawa wengi. Hivyo basi, hakikisha unafikicha akili yako vizuri kwenye kila kitu unachoambiwa na kuletewa.
njia pekee ya kuwa mtu unayetaka kuwa ni kujitahidi kuwa bora kuliko jana. Kila siku inapobadilika ina maana, baraka zake na kumbukumbu zake muhimu. Ipe maana njema hiyo kesho yako ili ufanikiwe kirahisi sio tu kwa maombi bali kwa kuwa na HEKIMA yenye BIDII!
hakuna mtu anayependa ufanikiwe kumzidi yeye, unafikiri atakwambia yote ili umzidi? Hebu uwe na akili basi! Hivi unawezaje kujilinganisha na mtu ambaye hujui kusudi lake wala malengo yake? Huoni kuwa huo nao ni ukichaa tu!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.