Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukweli mchungu ni kwamba,,, Jipambanie maana Watu watatoka mbali kuja kukuzika ila hawatotoka mbali kuja kukupa chakula ili usife njaa.
 
Mkumbushe mwanao kuwa kukaa kwenye meza wanayojadili mambo ya watu kuliko maisha yao binafsi hakutampa anachokitaka bali kutampotezea muda,dira na mwelekeo wake wa maisha.
 
Mkumbushe Mwanao ya kwamba..... Wakati mwingine ni bora MENGINE asitake kuyafahamu ili aendelee tu kubaki na amani katika MOYO wake.
 
Mkumbushe mwanao ya kwamba...... Kamwe asiruhusu mtu yoyote ambae hajawai kuvaa viatu vyake amfundishe namna ya kufunga kamba.
 
Haijalishi una machungu au furaha kiasi gani, Mungu anatosha kuwa Shahidi.Usimsahau Muumbaji.
 
Dunia haitaacha kusonga kwa sababu tumekata tamaa. Wajibu wetu ni kutembea kwa imani na subira, ikiwa na uzito wake kwa jasho na machozi.
 
MUDA ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu, ndio maana hatupaswi kuishi tukifungwa na makosa ya jana, bali tu tengeneze leo ili kesho iwe bora.
 
Kupitia maumivu tunajifunza mengi, kupitia machozi tunapunguza uchungu na kupitia changamoto tunapata hekima.
 
Usipime kina cha maji kwa mguu mmoja, Kama hujui jambo, nyamaza, uliza na ujifunze, Usiharakishe kusema bila maarifa, Utaanguka pasipo msaada
 
Usilaumu mtu yeyote kwenye Maisha, maana watu wazuri wanakupa furaha na watu wabaya pia wanakupa somo, watu Bora na wema wanakupa kumbukumbu nzuri
 
Kama unaguswa na maumivu ya watu wengine basi chukua hatua, sema hata kidogo, ili kuwakilisha sauti yao wale walioteswa.
 
Haijalishi giza linakuwa zito kiasi gani, asubuhi huangaza tu. Ndivyo ilivyo pia kwenye maisha yetu, changamoto, huzuni na majaribu havidumu daima.
 
Wanadamu wote tunaongezeka urefu sentimita moja kila asubuhi na kurudi katika hali ya kawaida kadri muda unavyozidi kusogea.
 
Si kila anae shangilia huko batani ni anafuraha hapana wengine huo ndio muda wao wa kupiga yowe na kujisahaulisha machungu yao
 
Mungu hatatuongoza mahali asipoweza kutuweka. Neema yake daima inatosha kwa ajili yetu katika hali yoyote na kila hali ya maisha yetu.
 
Hata kama umekasirika , fikiri kabla ya kuzungumza." Maneno unayosema yanaweza kusamehewa ila hayawezi kusahaulika.
 
Back
Top Bottom