Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_20251117-191504_Web Browser.png
 
haina haja ya kuumiza kichwa. Kwani mtu akikwambia hauna akili una haja gani ya kupoteza muda kuthibitisha kama kweli hauna akili? Ukikaa kimya utakuwa umepoteza nini? Vita nyingine ziache zikupite zitakupotezea muda wako bure
 
Kila wakati JIFUNZE KUOMBA kwani dunia hii inaendeshwa kwa KANUNI za KIROHO. Mungu anaweza kugeuza maisha machungu kuwa matamu! Mungu anaweza kugeuza ndoa chungu kuwa tamu tena, we omba! Mungu anaweza kugeuza tabia chungu kuwa tabia tamu tena, nasema omba tu!
 
usiibebe jana mbaya kwenda nayo kesho. Inawezekana ni kweli umefeli katika yote lakini haiondoi ule ujasiri wako wa KUJARIBU KUFANYA. Kufeli siyo kinyume cha kufanikiwa, kufeli ni mafanikio yenyewe.
 
kusema ukweli ni kuzuri pale tu ukweli utakaposemwa ukaleta faida lakini kama kusema ukweli kutaleta machafuko, basi kusema ukweli si kuzuri. Kama kusema uongo kutaleta amani basi kusema
 
siku ulipokuja tu hapa DUNIANI, ndio siku ulikubali kuwa wewe ni mkubwa kuliko MATATIZO yako. Matatizo yatakupima! Matatizo yatakupanga ili upangike vizuri! Matatizo ndio fursa yako kama utayatumia vizuri.
 
Ni kweli imethibitika kuwa waliofanikiwa sana ni wale WALIOFELI mara nyingi sana kwenye maisha yao. Yaliyotokea kubali tu yameishatokea. Huwezi kuyabadikisha. Mshukuru Mungu kwa darasa hilo halafu ANGALIA mbele unakokwenda kwa IMANI kubwa sana kwamba UTAFIKA TU
 
hakuna mwalimu mzuri sawa na muda. Muda ndio darasa la walimu wote. Muda ndio msema kweli katika dunia hii ya watu wanaopenda kuambiwa uongo tu. Muda ni HAKIMU mtenda HAKI usipingane nao. Muda hausemi uongo. Muda huweka hadharani yale yafanywayo NURUNI na GIZANI.
 
unateseka kuishi maisha ya kifahari huku wajua fika YANAKUTESA! Huo nao ni umaskini wa mali na akili. Hakika maisha ni kitendawili, tenda na ishi unavyoweza ili usijekufa kwa presha za maisha ya watu wengine bure!
 
Maisha Yako Wewe ni Yako Mwenyewe Na wewe ndio Utapanga Mwenyewe Uishije siku Zijazo Hamna Mtu anaweza kukuletea maisha Mazuri Bila wewe Mwenyewe Kupambana
 
Sekunde moja ikipita, zaidi ya milioni 100 za seli mwilini mwako zinakuwa zimekufa na nyingine mpya kuzaliwa
 
Back
Top Bottom