kama utachukua muda wa KUJITAHIMINI vizuri na ukasafisha madirisha ya macho yako ya ndani ili UONE VIZURI. Kuna mengi yatajifunua kwako! Kikubwa muombe sana Mungu akupe macho ya rohoni ili uone uzuri wa kitu kilichopo mbele yako.
Mungu siyo Mungu wa magumu tu, ni Mungu wa kila kitu kwenye maisha. Jifunze kusema nae wakati wote. Usikubali kufanyiwa UDALALI kwenye kujenga mahusiano yako na Mungu wako! Hakuna mtu anayemjua mtu zaidi ya Mungu na mtu mwenyewe!
wapo wengi ambao walianza kujenga taswira akilini mwao kwenye vile vitu walivyokuwa wanavitaka sana vitokee katika uhalisia. Wakayashikilia maono yao na hatimae wakafanikiwa kuprint vile vyote vilivyokuwa akilini mwao katika uhalisia na wakaibadilisha dunia
chochote kile utakachokifanya katika DUNIA hii huwa kina matokeo chanya na hasi. Kabla hujafanya chochote kile tambua kuwa wewe ni MBEGU, wema na ubaya vyote ni mbegu na vyote ukivipanda vinaota na mvunaji ni wewe uliyevipanda!
, pesa ni jawabu la mambo mengi maishani lakini sio kila kitu, huu usemi wa kwamba pesa siyo kila kitu, sawa lakini hakikisha unazipata kwanza ndio uongee huo upuuzi wako alisikika tajiri mmoja akisema. Ukiwa huna pesa hata ndoto unazoota zinakosa mpangilio.
Ukweli mchungu ni kuwa PESA inaleta utulivu wa akili, mwili, hadi roho ndio maana wanasema usimwamini mtu yeyote yule hadi ashike hela! Akiwa hana ananena kwa lugha bila mpangilio, akizipata anaongea Kingereza!
wakati wengine wanakuona mjuaji; usieeleweka wala kuaminika kupewa nafasi na msomi asiye na pesa. Wewe jiamini! Amini katika maono yako! Ishi maisha yenye kusudi. Na usikubali kuishi maisha ya UCHAWA hata siku moja!
kabla hujaamua kufungua mdomo wako hebu jiulize; Hiki nachotaka kusema kina umuhimu? Kina ukweli? Kitabomoa ama kitajenga? Kusema ukweli ni kuzuri pale tu ukweli utakaposemwa ukaleta faida lakini kama kutaleta machafuko, basi kusema ukweli si kuzuri!
Mafanikio huja kwa ule wakati sahihi uliopangwa na Mungu, cha muhimu jifunze kutembea kwenye wakati wako huku ukiomba sana Mungu akupe MISULI YA IMANI katika kutimiza kile ulichoamua kufanya kwenye maisha yako.
muda ukifika wa watu uliowapenda kukupika wala usiwachukie kwani ndivyo binadamu walivyo. Shule ya watu inatufundisha kuwa rafiki wa kweli kwenye maisha yako ni WEWE MWENYEWE kwanza. Hii itakusaidia kuishi kiasi huku ukijua fika kuwa kila mtu ipo siku ATAKUA
, ukikubali kuishi maisha yasiyo na maono ni kukubali kuishi kama kunguru! Utataka kufanya kila kitu; utataka upendwe na kila mtu; utataka ueleweke na kila mtu; utataka kudandia na kushindana na maono ya wenzako na mwisho wa siku utajikuta UMEFARIKI badala ya KUFA.
Elewa kuwa ulikuja hapa DUNIANI peke yako na utaondoka peke yako, litafute kusudi lako kupitia maono yako. Hakuna atayekusaidia kuyaelewa vyema maono yako zaidi yako, huwezi kuwawekea watu wengine presha ili wakusaidie kuyatimiza maono yako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.