Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanasiasa wa Kirumi Gaius gracchus, kichwa chake kilihitajika kwa malipo ya dhahabu sawa na uzito wake. Hivyo atakayemuua na kupeleka kichwa chake angepewa dhahabu sawa na uzito wa kichwa hicho. Hata hivyo dhahabu hii haikulipwa kwa mtekaji kwa sababu alikijaza kichwa hicho madini ya risasi ili kiwe kizito zaidi.
 
Kampuni ya kutengeneza midoli ya plastiki ya LEGO hutoa dhahabu gramu 25.65 kwa wafanyakazi waliotimiza miaka 25 ya utumishi katika kampuni hiyo.
 
Wanawake wa India wanavaa asilimia 11 ya dhahabu yote iliyoko duniani. Hiki ni kiasi cha zaidi ya kilichoko Marekani, Uswisi, Ujerumani na IMF zikijumuishwa kwa pamoja
 
Kipande au tofali kubwa zaidi la dhahabu duniani lina kilo 250. Tofali hili linamilikiwa na kampuni ya Mitsubishi, na linakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 3,684,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…