Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1766228740165.jpg
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya matunzo na malezi,na kwa
bahati mbaya sana siku hizi jamii inazingatia zaidi matunzo kuliko malezi.
 
Hakuna makofi. Hakuna sifa. Ni juhudi za kila siku tu.
Siku moja, matokeo yataongea kwa niaba yako.
 
Usibebe hofu za wengine kuwa hofu yako. Kila mtu ana safari yake katika hii dunia inawezekana safari yako ni ndefu kuliko ya huyo unaemuona bora.
 
Kinachotokea katika maisha ya watu wengine hakina uhusiano na maisha yako. Acha kukariri matatizo ya wengine kuwa ni matatizo yako.
 
Tabia njema inakufungulia milango ambayo hata elimu haifungui. Inakujenga mahali ambapo pesa haipatii nafasi. Inakuheshimisha mbele ya watu ambao hawakuwahi kukubali. Hata kimya chako kikiongea, kitaheshimiwa kwa sababu ya utu uliouchagua.
 
Kwenye safari ya maisha, Mungu atuweke mbali, na wale wanaoona negative kwenye kila kitu chetu..

Wale ambao tukiwabeba migongoni, wanasahau hadi umbali wa safari..

Tukiwaonesha upendo wetu, wanadai walishaupata kama huo hapo kabla, ukawaumiza..
 
Bila kujali ni Mambo mangapi magumu unayopitia, lazima utafute sababu ya kutabasamu, Maisha ni mafupi sana, ishi maisha yako, Sali, penda na kuwa tayari kwa kuondoka katika hii dunia.
 
Kila kinachochelewa si kukataliwa, na kila giza la usiku linaandaa mwanga wa asubuhi. Ishi ukiwa na amani moyoni kile unachokiomba kinafanyiwa kazi kimya kimya.
 
dunia inakuzunguka, lakini moyo wako ndio utakayekuwezesha kuona mbali. Usikubali tamaa iwe kikwazo, usikubali wivu ushike nguvu zako. Jifunze kwa wengine, lakini safari yako ni yako. Ni wewe pekee unaoweza kuandika hadithi yako.
 
Hakikisha kama unaweza kumsaidia ndugu yako wa damu fanya uwezavyo msaidie tu haijalishi ni mara ngapi wewe fanya hata bila kukumbuka ni mara ngapi ulimsaidia
Usiache asaidiwe na watu wengine kuna nguvu ya upendo inapungua.
 
Back
Top Bottom