Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pigania kesho yenye picha kubwa alafu ishi. Usipoteze tumaini,
Walio nyuma yako wewe ndio role model wao.
 
Usiishi kwa Tumaini la mwendawazimu kuwa lipo siku atakuwa tajiri kwa kulitegemea jalala.
 
Usipange lawama kwa kufelishwa bali panga mwelekeo mpya utakaowafelisha waliokufelisha.
 
Usiwapoteze watu ambao wapo kwa ajili yako kila wakati. Watu hao ni nadra sana kuwapata katika karne hii iliyojaa wabinafsi.
 
Kwenye maisha kuna muda huitaji mambo mengi ili uweze kukaa sawa unaitaji vitu viwili peke yake, uwezo wa kukubali kuanza upya na uwezo wa kusahau...,
 
Moja ya kosa kubwa la kuliepuka ni kujidanganya mwenyewe..

Mbaya zaidi ni kudanganya mtu/watu ili upate validation, kama una hali hii tambua unajizika mzima mzima.
 
Upambanaji sio kuhusu nguvu za mwili pekee, ni kuhusu moyo usiokubali kushindwa hata pale kila kitu kinapoonekana hakipo sawa.
 
Chai Isiwe Ya Moto Sana Ukashindwa Kuinywa Wala Isiwe Ya Baridi Sana Ikawa Kama Maji, Jifunze Kujithamini Kabla Hawajakutumia Watakavyo

Kuna Wakati Inabidi Uwe Na MSIMAMO, Ili Wajue Kwamba Huvumilii UPUUZI
 
Sadaka huanzia moyoni na si mfukoni. Toa kwa sababu moyo wako umeguswa na si kwa sababu mfuko wako umefurika. Sadaka yako haitapimwa kwa kiasi bali kwa imani".
 
Kabla ya kulalamika juu ya ladha ya chakula chako, fikiria mtu ambaye hana chochote cha kula.
 
Magazeti ya leo
IMG-20260102-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom