kila mtu ana hadithi yake, kila mtu ana mapambano yake. Usipige kelele kwa mafanikio ya jirani yako, bali tazama kama darasa la maisha. Jifunze kutoka kwao; jinsi walivyopigana, jinsi walivyovumilia, jinsi walivyoweza kuibuka. Hivyo utaongeza nguvu zako, si hasira zako
Wanaostahili ushindi ni wale , waliozishinda changamoto walizokutana nazo. Kama njia yako haina vikwazo , itazame tena ramani yako. Kama barabara yako haina hata mawe njiani , ichunguze tena safari yako.
Mwisho wa mwaka huwa na matumizi makubwa mengine hata sio ya lazima na mwanzo wa mwaka huwa na mahitaji mengi muhimu tena ya lazima,na shughuli ya kuchezesha mzani ni yako ,chezesha uwezavyo lakini hakikisha uzito unazidi kwenye mahitaji ya lazima.
Maisha haya ya kila siku yatakuchosha.Utakataliwa na watu uliowaamini. Utaambiwa maneno ambayo hata moyo haukuwa tayari kuyasikia. Utasalitiwa na wale uliowaficha ndani ya kina cha roho yako. Acha tabia yako iwe silaha ya kimya. Acha iwe ushindi bila vita.
Siku wewe ukifa itawachukua Wapendwa wako siku chache tu za kuishi kwa majonzi then wataendelea na maisha yao..Jitunze, Jipende na ukipata nafasi Jipendelee.
Ukishaamua kutoka nje ya nyumbani kwako, oga na pendeza jumla huwezi jua unakutana na nani uendako. Ukisema usioge tu ndio unakutana na wale watu muhimu ambao usingependa kukutana nao katika muonekano hafifu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.