Mtu anapokueleza siri zake za ndani na mambo yanayo muumiza anakueleza ili apone, kati yenu anatengeneza chumba cha uponaji hata kwako pia siku yako ikifika, lakini unapokwenda kuya sambaza kile chumba cha uponaji unakigeuza kuwa chumba cha umauti
Makosa, maumivu na magumu tuliyo pitia sio sababu ya sisi kukosa furaha, kutokuishi kwa amani na kufurahia maisha, dawa ya stori mbaya iliyopita ni kuandika stori nzuri ijayo
Makosa, maumivu na magumu tuliyo pitia sio sababu ya sisi kukosa furaha, kutokuishi kwa amani na kufurahia maisha, dawa ya stori mbaya iliyopita ni kuandika stori nzuri ijayo
Kuna wanao kuona upo chini ya mlima haujafanikiwa kwa sababu bado haujaanza hata kuupanda, but hawajui kufika hapo chini ya mlima umetoka kwenye shimo revu hadi kufika hapo juu ya ardhi chini ya mlima
Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili, zilizobaki apewe mgeni, yatima na mjane- katika kupata kwako usiwasahau walio kosa
Wacheki marafiki zako, pokea simu za ndugu zako, zungumza na wazazi wako, wazingatie uwapendao huwezi jua, inaweza kuwa ndio siku, wiki, mwezi au mwaka wa mwisho kuwa nao hapa duniani
Maisha yana mitihani ila Maisha yenyewe sio mtihani,hivyo hakuna anayefeli au kufaulu maisha,maisha ni uwanja wa mafunzo na elimu haina mwisho, walio pita walijifunza, tuliopo tunajifuna na wajao watajifunza,hakuna kufeli wala kufaulu bali kuna kuishi na kujifunza to enjoy vyote
Mtu ametumia miaka 40 kutafuta mali, akiondoka duniani kinafuata kikao cha siku moja kugawana mali zote na sio kuziendeleza kwa miaka 40 ijayo, watoto/wajukuu nao wanajikuta wanaanza moja.huu ni utamaduni wa kudumisha umaskini#generationalWealth
Ubebe mzigo wa changamoto zako au usubiri huo mzigo uje kukuangukia, umia kwa kuchagua kabla hujaja kulamizwa na maisha kuumia, kubeba mzigo kwa hiyari kuna saidia kujijenga kitabia na kisaikolojia, lakini mzigo wa kuja kulazimishwa na maisha unaitwa stress na ni mzito sana
Mapito yako ndio cheti chako cha kuja kuzibitisha ukuu wa Mungu pale atakuja kukufukisha akiwa amekuinua juu ya yote unayo pitia, hajakuacha bali anakujenga kiimani endelea kumwamini na kupambana
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.