Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dah! Sasa uandike wewe sawa! nikiandika mimi kosa! duh! umeshaachana na siasa za bongo lakini bado unaziandika badala ya kukaa kimya!
Hapana mkuu. Wewe andika tu. Hata ukiamua kuhamishia jukwaa zima la siasa huku ni sawa. Na kuachana na kitu na kukaa kimya juu ya kitu hicho ni vitu viwili tofauti - hasa kitu ulichoachana nacho kinapoletwa sehemu ambayo hukukitegemea au hakipaswi kuwa. Ukileta mambo ya dikteta uchwara huku, mara mgonjwa wa akili, mara hivi, usishangae kujibiwa hata kama wanaokujibu hawajali na hawana passion na uanaharakati uliotukuka kama wako. Ndiyo maana mambo haya ingefaa tu yaachwe huko huko Jukwaa la Siasa ili mtu akiyataka basi ayafuate huko akaoge matusi na kupambana katika vita visivyo na mshindi vya mafisi vs. manyumbu....
 
Mkuu SHIMBA YA BUYENZE nimekutilia likes Mkuu sina usongo nawe. Tanzania ni yetu sote Mkuu.
Na mimi moyo wangu ni mweupe kabisa. Ukiangalia notifications zako utaona likes zangu nyingi tu tangu uje kututembelea jambo ambalo kusema kweli limetupa heshima sana kwa sababu ma-great thinkers wa hapa JF siyo rahisi kujichanganya hivi na watu wa kawaida. Hata wakija kwenye majukwaa kama haya mara nyingi ni kuponda tu na kudharau. Not you [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122].

Vuguvugu la 2015 lilikuwa kali mno na baada ya kutafakari sana ndipo nikaamua kuachana na au niseme kutofuatilia sana mambo ya siasa hapa nchini. Wanasiasa wetu hawa wanabadilika badilika kama vinyonga na ukiwafuatilia sana aisee unaweza kukongoroka kisaikolojia na hata kiutashi unless uwe mwanaharakati kabisa na/au unafaidika nao kwa namna moja ama nyingine. Tuko pamoja mkuu...

Ubarikiwe mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…