Uzi maalum wa Maoni, Marekebisho na Changamoto kwenye Mfumo mpya wa IDRAS

Uzi maalum wa Maoni, Marekebisho na Changamoto kwenye Mfumo mpya wa IDRAS

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,436
Reaction score
4,756
Habari za wakati huu;
TRA Tanzania
Jana niliweka uzi hapa kuhusu changamoto ya IP blocking katika Mfumo mpya wa IDRAS
Nawapongeza kwa kufanya marekebisho na sasa naona computer za ofisini zinafikia ukurasa wa login.

Pamoja na marekebisho yaliyofanyika kuna tatizo JIPYA ambalo sasa linajitokeza:

Kwanz kabisa kuna wakati ile button ya login inaload na kusema inatafuta Security Keys.Hii ni feature ambayo haikuwepo mwanzoni.Tatizo sasa ni kwamba ikishafanya hivyo inalogin mara moja na kulogout kisha inasema session ended.Au inaweza fanya hivyo kwa muda mrefu na kisha kusema session timeout.

Wakati mwingine inlogin ila sasa inakupa error ya Loading Error "Resource Loading Error: Parameter"

Hii yote inamaanisha kwamba kuna maintenance work zinafanyika wakati watu wanaendeleakutumia mfumo.

Ushauri wangu.Kama mnatka kufanya aina yoyote ya Maintenance Jitahidini mzingatie Best Practices.

Kwanza kwenye IT huwa tunaambiwa IF it works do not change it.Kama unafanya kazi sawa Usiubadilishe.

Pili Hakikisheni mnafanya Maintenance wakati sahihi na mtoe taarifa ya DOWN TIME au limited Access hasa kama mnafanya LIVE maintenance ili yanapotekea changamoto basi muweze kuzishughulikia.

Mwisho Line zenu za Simu,Whatsapp,Social media na hata Njia za mawasiliano za kwenye Mfumo ni kama Vile zimekuwa hazina mtu anazisimamia.No response na Action.Kama watu wenu wanashindwa basi Mtumie hata AI kwa ajili ya kuufundisha mfumo wenu wamawasiliano badala ya kutokurespond kwa wakati.

Sio kila mara tunapata nafasi ya kuleta issues kama hizi ONLINE.

Wasalaam
 
Ni sahihi hiyo changamoto ya kushindwa ku log in hata mimi nimekutana nayo mara kadhaa,
Anyway changamoto kubwa kwangu kwa sasa nataka nifanye amendment katika portal yangu kwenye Corporate tax (income tax) hapa mwanzoni mwa mwaka nlijiwekea makadiro makubwa afu sasa kwavile biashara bado ni changa naona nimejibebesha mzigo mkubwa nataka nifanye mabadiliko ili hela nnayotakiwa kuilipa niweke ndogo ambayo naweza kui afford
Nimeongea na moja wa stuff wa TRA kaniambia natakiwa nifanye mwenyewe na hiyo access ipo ila mpaka sasa bado sijafanikiwa
 
TRA Tanzania Mbona kama hii hali inajirudia tena?Kama ni security feature mpya nafikiri mkubali kwamba haifanyi kazi mtafute mbadala wake.Same issue imejirudia tena Asubuhi hii
 
Back
Top Bottom