Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Asante mkuu ndo tunaanza na Corona hii
 
Hapa umemaliza kila kitu.
 
upo sahihi mkuu, ila kwa sasa leseni unaomba online, nilienda halmashauri ndio nikaambiwa hivyo, na mimi pia niliomba online, link hii hapa Home - TNBP

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi mkuu, ila kwa sasa leseni unaomba online, nilienda halmashauri ndio nikaambiwa hivyo, na mimi pia niliomba online, link hii hapa Home - TNBP

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi mkuu, ila kwa sasa leseni unaomba online, nilienda halmashauri ndio nikaambiwa hivyo, na mimi pia niliomba online, link hii hapa Home - TNBP

Sent using Jamii Forums mobile app
inategemea Mimi nilienda kuchukua leseni yangu mwezi mmoja uliopita pale mwenge karibu TRA, walinipa tu control namba kisha nikalipia CRDB na kurudisha ,baada ya siku tatu nikapewa leseni yangu....anahitaji Halimashauri ya manispaa wanapotoa leseni nenda hata pale mwenge mpakani utaona kontena lao.
 
1. Kupata TIN kwa mtu binafsi
Mhitaji wa TIN anaweza kwenda ktk ofisi za TRA zilizopo karibu na eneo analofanyia biashara kwa ajili ya usajili wa TIN ambapo atapewa fomu ya maombi na atajaza na kuambatanisha vielelezo vifuatavyo:
1. Barua ya Utambulisho wa makazi kutoka katika serikali ya Mtaa
2. Kitambulisho cha Taifa/Namba za kitambulisho cha Taifa kama haujapata kitambulisho
2. Picha 2 za passpoti saizi
3. Mkataba wa pango la sehemu ya biashara kama amepanga na kama hajapanga bhasi risiti ya malipo ya kodi ya majengo

Kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015, sect 35, Cap 438 mtu hy HUKADIRIWA KODI (Hajikadirii) na kuna viwango vya kulipa kodi vimewekwa kutategemeana na kama anaweka kumbukumbu au haweki. Kwa sheria mpya zilizoanza kutumika 2020, mauzo ya au zaidi ya mil 100 ataandaa hesabu za mizania (lazima kwn takwa la kisheria) na pia kumetolewa muda huru (grace period) ya siku 180 ambapo hatalipa kodi ya mapato kwa biashara mpya.

Kodi atakazolipa ni
A. Kodi ya zuio ya 10% ya thamani ya mkataba wa pango aliyolipa kama kapanga eneo la biashara
B. Ushuru wa stempu 1% kutokana na mkataba wa pango wa eneo la biashara alilopanga

B: Cheti cha Mlipa Kodi ie Tax Clearance Certificate
1. Mlipa kodi ataomba cheti hiki baada ya kukamilisha malipo ya kodi ya zuio na ushuru wa stempu
2. Mlipa kodi atasema Cheti kielekezwe kwenda manispaa/mamlaka ipi kwa ajili ya leseni

2. Kupata Leseni
Hili ni takwa la kisheria rejea Sheria za Leseni za Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 kifungu 3(a)
Kwa sasa mfumo unatambulika rasmi ni wa kuomba online kupitia tovuti ya biashara ie TNBP (japo kuna manispaa unaomba mfumo wa zamani). Lakini juu ya yote utaomba leseni kwa njia zote kwa kuambatanisha vielelezo hivi:
1. TIN (ulipata TRA)
2. TAX Clearance Certificate
3. Mkataba wa pango uliolipiwa kodi ya zuio na stempu
4. Kujaza fomu ya leseni no TFN 211 ya 2004 kwa zamani ila kwa sasa kuna data sheet mtandao utakupa mwongozo
5. Inategemea na aina ya biashara kwn kuna baadhi ya biashara utalazimika kuwasilisha vielelezo toka mamlaka nyingine za kuruhusiwa kufanya biashara

Regards

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni mambo ya kawaida tu boss. Wala usipanick. Kosa kubwa hapo ni huyo aliye kuandalia hesabu na sio TRA. Hakuwa muwazi kwako wa kukwambia kama uliwahi fanya imports au tin yako iliwahi kufanya biashara ya kununua gari au kadha wa kadha. Bila kufika mbali mtafute Tax consultant ambaye yuko smart akuambie ulikosea wapi. Baada ya hapo ongeeni nao TRA officers wawasaidie vipi. I hope you understand

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa sijakuelewa mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari yako mkuu.. Naomba kwa heshima na taadhima nikupe angalau ABC ya namna gani unaweza kukabiliana na hiyo hali. Na hapa pia nitajaribu kuweka wazi ili watu wengi na wanajamii forums angalau waelewe na hatimaye kuiamini au hata kuilewa TRA na majukumuku yake.
Kwanza kabisa nataka utambue kuwa.. WATU PEKEE WANAOTAKIWA KUANDAA VITABU VYAKO NI WAHASIBU WENYE CPA. usiende Kwa hao TAX CONSULTANTS hao kazi yako kubwa ni kukushauri namna ya kulipa kodi na kodi zipi ni halali na angalau wanaweza kujua zipi ni TAXABLE NA NON TAXABLE lakini hawajui namna ya kuandaa VITABU yaani FINANCIAL STATEMENTS by proffessional.
Pili nataka utambue kuwa hivyo vitabu vyako vitakuwa na vina some expenses ambazo kwa TRA lazima zikatwe kodi, yaan hurejeshwa ili kodi ikatwe then ucalculate hiyo profit yako.
Tatu nakuomba angalia mauzo yako yaan REVENUE kwenye INCOME STATEMENT YAKO NA LINGANISHA NA YA EFD machine. Any different inaleta faini ya 4.5 M. Lakini pia angalia gharama mbalimbali ulizotumia kuna zingine ziliondolewa kiuhasibu ili kupata hiyo faida lkn kwa TRA zinarudishwa ili kupata kodi halisi. LAKINI PIA KUTOWASILISHA RETURN ZA MIAKA MIWILI NI KOSA KISHERIA HIVYO WAO WATAKUKADIRIA KWANZA KWA MIAKA 2 HIYO NA ULIPO SASA HIVYO HIYO AMOUNT INAWEZA FIKA BILA SHIDA MKUU.
Nne angalia pia muda ambao ulifile return zako kama ulikuwa nje ya muda hapo pia kuna FAINI. Lakn pia kama kampuni unatakiwa ujue una wafanyakazi wangapi na kama wamefika 4 hapo unatakiwa kupeleka SDL na PAYE kwa kila mwezi na hapo ndio unaona sasa kodi ni kubwa kutokana na malimbikizo hayo. Lakin pia kama kampuni unatakiwa USAJILIWE VAT na kama hujasajiliwa kwa uzembe hapo unaweza pigwa offence na kupelekea kodi kuwa kubwa kiasi hicho.
USHAURI WANGU
Tafuta wahasibu wenye CPA wakuandalie mahesabu vizuri kupunguza hizo tofauti na usiogope kuwalipa vizuri maana ndio kazi yao. Sijaona haja uwape lawama TRA kwamba wanataka RUSHWA wakati hayo malipo HULIPWA KUPITIA BANKS NA WITH CONTROL NUMBER. Wewe rudi TRA waambie naomba muda nikarekebishe vitabu kwa kuangalia hints ndogondogo nilizokupa.
UTANISHUKURU BAADAE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeeleza vizuri ila hapo mwisho huo muda mchache wa kuipata leseni ni takribani siku ngapi kwa wastani
 
Huna akili!
Hasira za kutofikishwa kileleni umeona sehemu ya kuzimalizia ni hapa jf?
 
Safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…