Wadau, ushauri wenu ni muhimu sana hapa kwa mustakabali wa maisha yangu na familia yangu.
Moja kwa moja kwenye mada.
Ipo hivi, mimi nina kampuni ambayo kwa sasa sitaitaja kwa sababu suala bado haijaisha, mwaka 2018 nilienda TRA kufahamu taratibu juu ya ulipaji wa kodi za serikali. Walinikabidhi kwa wakala wao wa mahesabu (tax consultant) kwa kuwa kipindi hicho sikuwa na mhasibu. Wakala huyu alianza kutengeneza hesabu za miaka miwili 2017 na 2018, baada ya kukamilisha hesabu za miaka hiyo miwili alonionyesha kiwango cha kodi nachotakiwa kulipa kilikuwa jumla ni millioni 5.8, hivyo nilisaini mahesabu Yale na akayapeleka TRA.
Sikujua kama TRA watapitia tena mahesabu yale kama taratibu zao zinavyowataka wanaita assessment, hivyo baada ya kuyapitia walisema ninatakiwa kulipa kodi ya Tshs millioni 45.3, kwa kweli nilishangaa sana hivyo niliamua kuwaona ili nijue tofauti kubwa kiasi imesababishwa na nini. Walinitaka niende na tax consultant wangu ili watupe maelezo, lakini cha ajabu huyu tax consultant alikataa kwenda TRA na kwa ujumla hakuonyesha ushirikiano kabisa juu ya hili suala, na mimi sina uweledi wowote wa masuala ya kihasibu.
Niliamua kuwaandika barua TRA kuwajulisha kuwa hayo mahesabu siyatambui na nahitaji muda zaidi niyapitie na wakala mwingine wa TRA (tax consultant) mwingine ambaye nilimchagua mwenyewe. Cha ajabu TRA walinikatalia ombi langu na kumtaka tax consultant wa awali arekebishe hizo hesabu, tulipewa muda kama wiki moja.
Alipomaliza kurekebisha na kuzirudisha tena TRA ili ziendane na mahesabu ya awali, ilishindikana na nilitakiwa kulipa kodi ileile ya 45.3 million, pia wamenipa mwezi mmoja niwe nimeshalipa la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.
Kwa kifupi, kampuni ninayoiongoza ni mpya na haijawahi kuwa hata na Tshs 5 millioni bank, hivyo kwa ujumla hivyo kodi haiwezi kulipika. Wamesema kama sikubaliani na hivyo kodi inabidi nikate rufaa kwa kamishna wa TRA kwa sharti la kulipa theruthi ya kodi ninayodaiwa ambayo ni Tshs 15.1 millioni, ambazo pia hazilipiki maana kampuni haina uwezo wa kulipa ili rufaa isikilizwe, hata hivyo nimekosa imani kabisa na hawa TRA kwa sababu hata hivyo rufaa nikikata sina imani kama nitafanikiwa.
Nauliza hivi: Haiwezekani nikafungua kesi kwenye mahakama zetu za kawaida kuomba hesabu zirudiwe upya na kusitisha utekelezaji wowote kutoka TRA? Au ni njia gani nzuri naweza kutumia ili nijiepushe na hili janga?
Naombeni ushauri wenu kwa wale waliopitia suala kama langu au wale wanaofahamu wanishauri nini nifanye, naomba samahani kwa makala ndefu, japo nimejitahidi kuifupisha.
Sent using
Jamii Forums mobile app