Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Mkuu unadaiwa kwa maelezo yako na majibu hapo juu pia ni rahisi tuu nenda TRA wape namba ya Tin yako utaona kama unadaiwa au laa na kama una uhakika wa kufunga biashara nenda na barua ya Serikali za mtaa na yako ya kufunga ila deni lipa ili lisiendelee kusoma...
 
Kwahio sasa hawa jamaa watanidai kwa mfumo gani kama nikisema nakacha? Maana kufungua biashara kwa TIN sidhani kama nitarudia upuuzi huo!
 
Kalipe Deni mkuu na hakikisha umebadili iyo TN vinginevyo bado utasomeka mlipa Kodi! Kumbe adi TN ulibadili huwezi kuwa na TN ya biashara kama hufanyibiashara! Me nilifunga biashara sikubadili TN wakawa wananitumia msg za kwenda kulipa kodi nilivyo ona msg zimezidi nikaenda nikaambiwa nina daiwa nikawapa barua zao na za serekali za mtaa za maombia ya kufunga biashara wakarudisha kumbu kumbu saw a maana nao ata kama wana juwa na wewe huna kumbu kumbu za maandishi watakupiga rushwa au vyovyote vile!
Wanadai kuwa ni lazima u convert tini ya Leseni ile ile inafanyika kuwa ya biashara ndio upate TIN kwa ajili ya kuombea Leseni ya biashara. Sema mi TIN yangu bado inasoma vile vile kama nilivyosajili awali ila haisomi jina la biashara wala location.
 
Nmeongea na Cousin wangu yuko HQ ameniambia ni kweli ile laki ntadaiwa pamoja na penalties ila hawana control nayo hivyo kunisumbua sumbua na kimashine chao cha kishenzi hawataweza ila amedai nipeleke barua za kufunga biashara tu toka serikali za mtaa.

Kwahio penalty zita stop niki report kufunga biashara.
Kama biashara umeifunga hawawezi kukutafuta ukalipe deni.
Achana nao..
wakikutafuta waambie umefunga sababu ya corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivi utakuwa unadaiwa.Kamalizane nao in peace.
sidhani kama situation zina match ila ni kwamba nili convert TIN toka driving Licence na kuwa ya biashara kisha nikafanyiwa mahojiano mafupi tukafikia kwenye form flani ambayo walitaka nikalipe laki maana ndio biashara imeanza sijaanza kukadiriwa rasmi.

Mi kwa kuona ni mwisho wa mwaka nikaona siwezi lipia biashara december laki hela ya mwaka mzima halafu mwezi wa 3 nilipe tena laki ingine ya mwaka mzima.

Nikauchuna hadi mwezi wa 3 ambapo pia sikulipa baada ya mlipuko wa Corona.

Sasa hapo ndio napanga nipotezee au nifanyaje ili kuepuka soo kama kutakuwa na kufuatiliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa uelewa wangu baada ya mahojiano walikuprintia fomu ya malipo ya laki moja uende ukalipie benki au kwa wakala siyo? Kama ni hivyo walishaingiza taarifa zako kwenye mfumo wa TRA. Ilitakiwa usiende kabisa au ujifanye umekuja kupata taarifa za nini ufanye ili upate leseni. Kwa kifupi unatakiwa kulipa hiyo laki pamoja na penati na uwajulishe pia umefunga biashara la sivyo hiyo TIN itaendelea kuonekana inafanya hiyo biashara uliyofanyiwa makadirio.
Umeelewa Kama nilivyoelewa!
 
Kwahio sasa hawa jamaa watanidai kwa mfumo gani kama nikisema nakacha? Maana kufungua biashara kwa TIN sidhani kama nitarudia upuuzi huo!
Labda usifungue biashara kwa TIN tena, lakini ukitumia TIN hiyo au ukiomba nyingine deni Hilo litasoma kwani TIN ina alama yako ya kidole!
 
Tayari umekwisha ingia kwenye system unacho takiwa kufanya ni kuandika barua ya kufunga biashara yako ila hayo malimbikizo utayalipa unless ukaongee nao kama wata kusamehe au vinginevyo.
Wakuu natumaini mko poa

Hapo awali nilikuwa napiga biashara ila sikukata leseni wala kitambulisho cha mjasiriamali. Ila kuna siku mapolisi walilengeshwa wakaja kunipiga hela (fine) kwa kigezo sina leseni na nina operate masaa ambayo hayajaidhinshwa kwa mujibu wa leseni ya biashara niliokuwa naifanya maana ilibidi kufungua kuanzia saa 9 alasiri.

Hii situation ikanifanya nika-process leseni ila ule mchakato sikuumalizaga, niliishia kuchukua application form ya pink ya manispaa kisha baada ya kuijaza wakaniambia niende TRA kupata Tax Clearance. TRA nilienda kweli nikapewa form flani yenye control number nikaambiwa nikalipie laki 1 baada ya mahojiano mafupi juu ya biashara.

Kimsingi ile laki sikulipa maana ilikuwa december ambapo nikaambiwa ntarudi tena mwezi wa 3 kulipa tena. Nilichekecha akili nikaona kile kitu ni kama kulipia kiingilio cha disko saa 12 kasoro alfajiri. Nikasema ntalipa mwezi wa 3 ili kama ni charge ya mwaka mzima basi iwe hivyo.

Kwa kifupi ile biashara nimeifunga sasa nawaza je, kwa hiyo scenario mamlaka ya mapato itakuwa napaswa nikajisalimishe tena na kuwaambia biashara nimefunga na watanidai zile hela ambazo sijalipia kwenye ile form au nipotezee niendelee na harakati zingine nile kobis?

NB: Mchakato wa leseni sikuukamilisha maana sikurudi tena manispaa nilibaki na form yao tu ya kuomba leseni na ile Tax clearance form ya TRA ila nilicholipa ni hela za usafi wa mazingira kwa serikali ya mtaa tu.

Yaan hapo mzee baba lazima ulipe na pia ulipofunga biashara ulitakiwa uandike barua,

born to shine
 
Naomba tueleweshane kuhusu namna ya kufungua biashara rasmi hasa hizi biashara ndogo ndogo na kwa hili ninaomba kama kuna tax experts or TRA Oficérs humu wanisaidie. Wiki hii nimeenda kufungua biashara yangu ndogo( ya duka ofcourse) kama wanavyoelekeza waliniambia nikachukue TIN ndipo nije nikate leseni.

Nimewahi kusikia matangazo mengi kwamba TIN ni bure lkn haikuwa hivyo kwangu. Bàada ya kukamilisha taratibu zote za kupewa TIN niliambiwa nilipie rental fee 24,000 na stamp duty(10% ya rental) 2400 Jumla 26,500 ndipo niweze kupewa tax clearance niweze kwenda kukata leseni.

Sasa naomba kwa wataalamu wanaojua utaratibu huu vzur wanieleweshe kwanza maana ya rental fee( maana nilipomuuliza afisa aliniambia hii ni kodi ya pango nikamuuliza sasa kama ni kodi ya pango ninalipaje TRA mmenipangisha wapi? Akasema hii ipo na nilazima kwa biashara zote mpya).

Mbili kama kweli ipo na ni halali naomba kujua namna wanavyoi calculate maana hakuna maelezo yoyote yalionyesha wameicalculate vipi mpaka kuja hicho kiasi. Ntashukuru kwa maelezo na ushauri wowote. #Pamoja tunajenga Uchumi na Taifa letu.
 
Naamini katika requirements walizokwambia upeleke ni Mkataba wa Pango/eneo la biashara
Katika mkataba huo sasa wataweka 10% ya kodi ambayo imelipwa;

Hii 10% (24,000) ni Withholding tax on rent na hiyo (2400) stamp duty ambayo inatofautiana sasa;
Stamp duty itatumika kama mbadala wa risiti ya Mwanasheria kwenye mkataba huo wa pango ambapo kila mkataba unatakiwa ufanyiwe kitu kinaitwa "Attestation" na mwanasheria na kwa wanasheria wengi ili wakupe risiti inabidi ulipie 20,000/-

NB: Mimi sio mwanasheria wala mfanyakazi wa taasisi yeyote ya Serikali/Kifedha; Maelezo haya nayatoa kutokana na taarifa, muongozo na experience nilizopata katika safari yangu ya kuanzisha Biashara miezi michache iliyopita

Kwa kifupi ni hivi

1. Biashara zisizolipa kodi
Kwa mujibu wa sheria ya kodi (TAA 2014 Sect. 35, CAP 438) kuna viwango vya mauzo vilivyowekwa ambapo mfanyabiashara binafsi atatakiwa kulipa au kutolipa kodi.

A: kutolipa kodi
Mauzo yakiwa chini ya mil 4 kwa mwaka mfanyabiashara hy binafsi hatalipa kodi

B: Kulipa kodi
Mauzo yakiwa zaidi ya mil 4 kwa mwaka atalipa kodi kutokana na kiwango cha mauzo aliyouza/anayotarajia kuuza baada ya kufanyiwa 'assessment na afisa wa kodi'

Note: Serikali imetoa muda wa siku 180 huru (grace period) kwa biashara zinazoanza hadi kuja kuanza kulipa kodi

C: Je kodi zipi ni lazima kulipa hata kama upo kundi la kutostahiki kulipa kodi ie kundi A?
Kuna kodi ambazo mfanyabiashara huwajibika kulipa kodi hizi either kwa yeye mwenyewe au kwa niaba ya mwingine kisha kukata hiyo hela. Kodi hizo ni:

1. Kodi ya zuio ie withholding tax (rental fee)
Hii ni kodi inayokokotolewa kutoka ktk mkataba wa pango kwa mtu aliepanga eneo la biashara. Ukokotoaji wake ni jumla ya hela uliyolipa kwa muda huo ktk mkataba kisha zidisha kwa 10%. Kiwango kinachopatikana ndiyo kitakacholipwa. Kodi hii hustahiki kulipa MNUFAIKAJI ie mwenye eneo la biashara. Hivyo bhasi wewe unamlipia kisha unatakiwa umkate kiasi ulicholipa na kumpa risit ya malipo ya TRA uliyolopia kwa niaba yake. Ktk maelezo yk hapo ina maana walifanya hesabu ya 20,000 kodi kwa mwezi *12*10% =24,000

2. Ushuru wa stempu
Hii ni kuhalalisha kisheria mkataba wako wa pango ambao wewe uliwaambia umepanga. Ni 1% ya jumla ya tozo ya kodi uliyolipa ie 20,000*12*1%=2,400. Anaestahiki kulipa ushuru wa stemp ni wewe mfanya biashara kwa sababu unauhalalisha mkataba ule
 
Lakini mbona hakuniomba mkataba wa pango aliniuliza tu ni wap unapofungua na mtaji wako ni sh ngapi
baada ya kumpa vielelezo vyote vya serikali ya mtaa?
 
Happy kwenye kumkata baba mwenye pango akikataa nachukua hatua zipi?
 
Back
Top Bottom